Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

(a) “Mame Bakari” Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka. (alama 10)
(b)“Masharti ya Kisasa” “…mapenzi ni mateso,ni utumwa, ni ukandamizaji , ni ushabiki usio na maana.” Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi. (alama 10)

 (7m 37s)
9182 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
(a) “Mame Bakari”
Kwa mujibu wa hadithi hii, ubahaimu anaotendewa mwanamke unakuwa na athari mbaya kwake. Onyesha kwa mifano mwafaka. (alama 10)
-Tukio la kubakwa linampotesea fahamu na anaaibika sana anapozinduka na kujipata akiwa uchi uk 47
-Mwanamke kujeruhiwa – Baada ya Sara kubakwa na
janadume lile, anaharibiwa na kuvuja damu.
-Mwanamke kuvunjiwa ujanajike na utu wake.
-Maisha ya mwanamke kuingiliwa na kuharibiwa.
-Mwalimu mkuu hamsikilizi wala kumhurumia – badala yake aliongoza kumkejeli na kumweleza ile haikuwa shuke ya wazazi bali wa wasichana.
-Mwanamke anateseka kiakili – Sara anaingiwa na mawazo
mengi jinsi atakavyoukabili ule ujauzito.
-Mwanamke katika umri mdogo anabebeshwa mimba jinsi Sara alivyofanyiwa.
(b)“Masharti ya Kisasa”
“…mapenzi ni mateso,ni utumwa, ni ukandamizaji , ni ushabiki usio na maana.”
Thibitisha ukweli wa kauli hii kama unavyojitokeza kwenye hadithi. (alama 10)
-Mtahiniwa azingatie masharati ambayo mwanamume anafaa ayazingatie pamoja na athari zake katika maisha ya ndoa.)
-Dadi ndiye mchuma riziki-yeye ni muuza samaki na apatacho kinatumiwa kuilisha jamaa yake.
-Dadi anasaidia kazi za nyumbani lakini mkewe Kidawa hatosheki na hayo.
-Kidawa hakubali kuwa mwanamume kazi ni za nje si za ndani na kuwa Dadi kufanya
kazi za ndani ni hisani tu. Uk 60.
-Dadi analazimika kushika shughuli za upishi kama vile kukuna nazi na kutia mboga tui.
-Dadi anaosha nyumba, kufagia, kufua na hata kupiga nguo pasi.
-Wanandoa kujiwekea masharti ya uzazi. Wanahiari kumzaa mtoto mmoja tu kutokana na athari za usasa.
-Dadi hataki mkewe atembeze bidhaa za kuwauzia wateja. Kila mara mkewe anapofanya hivyo, anaumia sana. Anaiona hiyo kama fursa ya mkewe kuhusiana na wanaume wengine . Uk 61.
-Dadi anaona ugumu wa masharti ya mkewe katika maisha ya ndoa lakini anashinda kumweleza.


|