Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

(a) Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika tumbo lisiloshiba (alama 10)
(b)Dhihirisha ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo (alama 10)

 (11m 1s)
3880 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
(a) Jadili matatizo yanayowakumba wakaazi wa Madongo poromoka katika tumbo lisiloshiba (alama 10)
i. Wanamadongoporomoka wanadharauliwa na kutwaliwa ardhi yao
ii. Kuporwa ardhi :ardhi yao imenyanyaswa na tabaka la mabwanyenye .
iii. Wanawatoa katika ardhi yao kuvunja vibanda vyao pasipo hata kuwalipa fidia.
iv. Unyanyasaji huu unafanya kwa wakazi hawa kwa kuwa hawana mtetezi.
v. Haki imenunuliwa na wenye nacho.wanabomolewa vibanda vyao ilhali hawajaonyesha mahali mbadala pa kwenda kuishi.
vi. Ukosefu wa haki :watu wa madongoporomoka hawana haki wenye fedha wanawaona wakazi hawa kama takataka tu.
vii. Ardhi ya madogoporomoka inaponyakuliwa na wenye
nacho wanashindwa kupata mtetezi.wanasheria wamenunuliwa na matajiri.ni vigumu kupata mwanasheria mwaminifu.
viii. Makazi duni:wakazi wa madongoporomoka wanaishi katika makazi yenye mandhari chafu.
ix. Wanaishi katika vibanda uchwara vinavyozungukwa na uozo na bubujiko la maji machafu.
x. Wakazi wa madongoporomoka wananyimwa fidia inayolingana na thamanni ya makazi yao waliyopokonywa na mabwanyenye.
xi. Watu wa madongoporomoka wanaachwa njaa baada ya jitu kubwa kula chakula chote.
xii. Wakazi wa madongoporomoka wanabaguliwa. Sehemu
wanaoishi hakuna maendeleo yoyote.
xiii. Wanamdongoporomoka wamekosa usalama.wanaishi kwa wasiwasi sana.wanaamshwa kwa vishindo vya mabuldoza.
(b)Dhihirisha ukweli wa methali “mzoea sahani vya vigae haviwezi” katika hadithi ya mapenzi ya kifaurongo (alama 10)
i. Mtu ambaye ni tajiri mwenye kuzoea kuwa na mahitaji yote maishani kama penina itakuwa vigumu kuishi kwa taabu na hali ambayo kila kitu ni duni.
ii. Penina Anatoka katika familia yenye nafsi kifedha, hivyo hakosi mahitaji yake yote.
iii. Dennis ni mtoto wa fukara ambaye amekosa mahitaji yake ya msingi. Hata chakula anapata kwa shida sana.
iv. Dennis anaona haitawezekana kuwepo na mahusiano mwafaka kati yake na Penina.
v. Penina anasisitiza kuwa inawezekana kabisa msichana wa kitajiri atangamane na kijana mwanaume ambaye ni fukara.
vi. Penina anafanikiwa kumshawishi Dennis kwamba hilo linawezekana na wanaanza kuwa na uhusiano wa kimapenzi.
vii. Waliahidiana kuwa wangefunga ndoa baada ya kuhitimu masomo yao na kupata kazi.
viii. Walishirikiana vema na wakaonyesha mapenzi moto moto mithili yao ulimi na mate.
ix. Walipomaliza masomo waliamua kuishi pamoja katika nyumba ya kupanga. Kila kitu waligharimiwa na wazazi wake Penina.
x. Baadaye changamoto inaibuka wakati Penina
anapodai kuwa hawezi kuolewa na mwanaume ambaye hana kazi yenye mshahara mkubwa.
xi. Penina anamvumilia Dennis kwa muda wa miaka mitatu na hatimaye uvumilivu unamshinda.
xii. Ahadi zote ambazo Penina alimuahidi Dennis zikaanza kuota mbawa.


|