Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Mhini na mhiniwa njia yao moja. Jadili ukweli wa methali hii ukirejelea hadithi ya mkubwa (alama10)

 (8m 7s)
6085 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mhini na mhiniwa njia yao moja. Jadili ukweli wa methali hii ukirejelea hadithi ya mkubwa (alama10)
-Mtenda maovu na mtendewa maovu wote huathirika vibaya
-Hadithi hii inarejelea namna viongozi wakubwa serikalini wanavyotumia nafasi zao katika kufanya biashara ya dawa za kulevya
-Mkubwa alikuwa na tamaa ya utajiri akawania uongozi ili
apate pasipoti ya kidiplomasia ambayo inampa nafasi ya kutokaguliwa katika viwanja vya ndege.
-Mkubwa anashinda uchaguzi na kupata cheo hatimaye anapata pasipoti ya kidiplomasia
-Anaitumia kupitisha dawa za kulevya bila kukaguliwa. Mkumbukwa ndiye aliyepokea shehena ya unga
-Mkumbukwa anakamatwa na kupelekwa kizuizini, huko
anaambiwa na mahabusu wenzake juu ya athari ya dawa za kulevya baadaye anatolewa na mkubwa
-Mkumbukwa anafanya maamuzi ya kuachana na biashara hiyo.
-Anamwonya na kumlaani mkubwa kwa kuangamiza vijana wa Mchafukoge
o Kisadfa mkubwa akiwa katika ndoto, anaona vijana wanavyoteseka baada ya kuathiriwa na dawa za kulevya
-Vijana wengi walikuwa wezi na kuchana nyavu za nyumba
-Miongoni mwao wapo watoto wake wa kiume
-Anapotoka usingizini anachuna majani ya miti na kujitwika kichwani
-Vijana waliotumia dawa za kulevya aliwahini na kuwatendea maovu watoto wa wengine hivi sasa hayo maovu yanamdhuru yeye
b) thibitisha kuwa ulitima ni kati ya maudhui ya hadithi ya mkubwa (alama 10)
Ulitima maana yake umaskini au ufukara
-Mhusika mkubwa alikuwa maskini sana. Mweruli aliokuwa nao ulikuwa umekatika mfumbati na kung’oka misumari mitatu
-Gari aliloabiri mkubwa lilipita Madongoporomoka sehemu ya wachochole
-Alipitia vichochoro vyenye vijumba vikongwe kudhihirisha umaskini
-Biashara ya kukaanga pweza ilikuwa yenye pato dogo tu
-Wakati alipomwelezea Mkumbukwa nia ya kugombea uongozi alimweleza kuwa anahitaji kuingia siasa ili kuachana na umaskini
-Watu waliompigia kura walipewa sukari,unga, kanga au mchele kuashiria umaskini
-Maisha awali ya mkubwa yalikuwa maisha duni hata kupata chakula ilikuwa shida
-Mkubwa hakuwa na mavazi alivaa nguo zilizojaa viraka


|