Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Ulezi umewapa wazazi wengi changamoto nyingi. Ukirejelea hadithi ya shogake, dada ana ndevu dhihirisha ukweli wa kauli hii (Alama 10)
a. Fafanua changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya Masharti ya kisasa (Alama 10)

 (8m 7s)
3496 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Ulezi umewapa wazazi wengi changamoto nyingi. Ukirejelea hadithi ya shogake, dada ana ndevu dhihirisha ukweli wa kauli hii (Alama 10)
– Safia anaonyesha tabia nzurimpaka anasifiwa na wazee wake Bwana Masundi na Bi. Hamida
-Wazazi wa Hamida walielewa fika kuwa kuzaa mwana si kazi, kazi ni kumlea
-Wazazi wengine walijalia watoto wao lakini wakawa balaa
-Mtoto wa Habiba Chechei, mkadi ana vitendo viovu
-Safia alifanya bidii masomo, kuheshimu watu na kuwasaidia wazazi wake kazi za nyumbani
-Wazazi wa Safia waliona rafiki wa Safia lazima awe kama Safia awe na tabia nzuri
-Safia na rafikiye Kimwana wanajifungia chumbani ili
kupata wakati mwafaka wa kusoma
-Safia alipoanza kutapika na kunyongonyea, mamake alipomuuliza, Safia alikasirika na kumlaumu mamake
-Babake Safia Masundi aliona Safia hawezi kuwa mjamzito.
a. Fafanua changamoto zinazokabili asasi ya ndoa ukirejelea hadithi ya
Masharti ya kisasa (Alama 10)
-Kwa kuwa Dadi alimpenda kidawa alikubali masharti ya kisasa bila kuyaelewa
-Kidawa kufanya kazi za umetroni kunafanya asimwamini
-Ncha nyingi za maisha zinamfanya Kidawa atembeze bidhaa za uarabuni mitaani
jambo lililozidisha shauku ya Dadi
-Dadi alichukia kujipamba kwa Kidawa akiona anafanya hivyo kwa minajili ya mwalimu mkuu
-Dadi pia alichukia namna Kidawa alivyosimama na kuongea na wanaume
-Bi Zuhura alimkejeli Dadi kwa kumtaka amparalie samaki
-Dadi aliogopa kuambiwa kuwa yeye si mwanaume tosha
-Maneno ya watu yalimfanya Dadi aache kusaidia kazi za nyumbani
-Dadi alimfuata Kidawa hadi shuleni kubaini kama Kidawa alimwendea kinyume na mwalimu mkuu


|