“ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.
Answer Text: “ Wahusika katika hadithi shibe inatumaliza wanatumia uhuru wao vibaya.” Onyesha ukweli wa kauli hii kwa kutoa mifano.-Mzee Mambo anatumia uhuru wa cheo chake serikalini vibaya kwa kupokea mishahara kutoka wizara mbalimbali ilhali hafanyi kazi yoyote.-Sasa na Mbura wanatumia uhuru wao vibaya kwakupanga na kupangilia wapi kwa kudoea badala ya kushiriki katika shughuli ya ujenzi wa jamii.-Wananchi wa taifa la Mzee Mambo wanatumia uhuru wao vibaya kwa kuzingatia kwenda kazini bila kujali kama wanafanya kazi yoyote. Muhimu si kwenda kazini ila kufanya kazi.-Mzee Mambo anatumia uhuru wake vibaya kwa kutumia mali na wakati wataifa kuandaa sherehe zisizo na msingi wowote. Anaandaa sherehe kubwa kwa madai ya kusheherekea kuingizwa kwa mtoto wake “nasari”.-Mambo anatumia magari ya serikali kuhudumu katika sherehe yake.-Walaji katika sherehe ya kuingizwa kwa mtoto wa kwanza wa Mzee Mambo nasari wanatumia uhuru wao wa kula vibaya kwa vilehawachunguzi kile wanachokula.-Vyombo vya habari vinatumia uhuru wao vibaya kwa kupeperusha sherehe ya kibinafsi moja kwa moja, badala ya kumulika mambo yanayoathiri taifa.-Sasa na Mbura wanatumia uhuru wao wa kula kila kitu kibaya na kizuri, wanachokijua na wasichokijua, vyao na vya wenzao hata vya kuokotwa.-Dj na wengine wenye nafasi katika taifa wanatumia uhuru wao kupokea mabilioni ya pesa za serikali kutumbuiza katika sherehe za mtu binafsi.-Dj na wenzake wanatumia uhuru wao kupata huduma za maji, umeme, matibabu miongoni mwa huduma nyingine bila malipo huku wananchi wakilazimika kulipia huduma hizi kwa dhiki na ufukara.