Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

‘… lakini shogake… shogake… shogake dada nikamwona ana ndevu.’
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Bainisha sifa tatu za ‘shoga’ anayezungumziwa katika dondoo hili. (alama 6)
c) Jadili umuhimu wa ‘dada’ anayerejelewa katika kuendeleza dhamira ya hadithi. (alama 10)

 (6m 6s)
4290 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
‘… lakini shogake… shogake… shogake dada nikamwona ana ndevu.’
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
Haya ni maneno ya Lulua.
Anamwambia mamake Bi.Hamida.
Wamo nyumbani mwao wakila chamcha. Lulua anamweleza jinsi alivyoingia katika chumba cha
Safia na kumkuta akiwa amelala kitandani na Kimwana.
b) Bainisha sifa tatu za ‘shoga’ anayezungumziwa katika dondoo hili. (alama 6)
(i)Misri-Wazazi wake Safia hawakuwahi kuiona sura yake kwa sababu alipenda kuvaa buibui ili asijulikane kuwa ni mwanamume.
(ii)Mzinifu-Anazini na Safia na kumpachika mimba.
(iii)Mjanja-Anajifunika buibui na kujifanya jinsia ya kike.
c) Jadili umuhimu wa ‘dada’ anayerejelewa katika kuendeleza dhamira ya hadithi. (alama 10)
-Dada anayerejelewa ni Safia.Ana umuhimu ufuatao:
(i)Ametumiwa kudhihirisha maana ya methali:mtu huvuna apandacho.
(ii)Ni kiwakilishi cha uozo katika jamii.Anawahadaa wazazi wake kuwa Kimwana ni shogake kumbe ni mpenziwe wa kiume.
(iii)Ametumiwa kukosoa malezi ya wazazi.Wazazi wake Bwana Masudi na Bi Hamida walimwamini sana hadi wakawa wanamsifu tu badala ya kuzungumza naye ili kumpa mwelekeo ufaao maishani.
(iv)Ametumiwa kubainisha maana ya methali:`Si vyote ving’aavyo ni dhahabu.
(v)Kuendeleza maudhui ya elimu.Alikuwa mwerevu shuleni.Kila mtihani alioufanya aliongoza katika darasa lao.


|