Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Jadili ufaafu wa anwani Tumbo Lisiloshiba kwenye hadithi hiyo. (alama 20)

 (6m 42s)
13135 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Jadili ufaafu wa anwani TUMBO LISILOSHIBA kwenye hadithi hiyo. (alama 20)
Anwani ya Tumbo Lisiloshiba ni mwafaka kwa Hadithi kwa Hadithi fupi ya TUMBO LISILOSHIBA. Anwani hii imetumika kijazanda kuashiria ile hali ya kutotosheka na alichonacho binadamu. Mathalan, mtu anaweza kuwa na mali, rasilimali, cheo fulani na kadhalika; lakini akawa
hatosheki kamwe, anataka aendelee kumiliki vitu zaidi na zaidi bila ya kuonyesha kuridhika kamwe. Anwani hii inadhihirika kwa jinsi zifuatazo;
Tumbo la jitu halishibi kamwe. Jitu hili linakula vyakula vyote kwa hoteli ya Mzee Mago, lakini halishibi kamwe. Baadhi ya vyakula vinavyoliwa na jitu hili ni kama vile wali, nazi, mchuzi wa Nyama, Nyama ya kuchoma kwa mkaa,
kachumbari, samaki wa kukaanga, chapatti n.k
Kudhihirisha kwamba jitu hili hajashiba, jitu lenyewe linamwahidi Mzee Mago kwamba litarudi katika mkahawa ule usiku inayofuata na linataka lipate chakula marudufu kushinda kile cha hivi leo. Kwa hakika, yanaonekana wazi kwamba tumbo la jitu hili halishibi kamwe.
Kadhalika, tumbo la wakubwa ambalo hapa limetumiwa kijazanda halishibi katika upande wa kujitaftia rasilimali zao. Licha ya viongozi hawa kuwa na mali na rasilimali kochokocho huwa wanataka wapate mali nyingine zaidi. Jitu na wenzake wakubwa wanataka wajenge majengo ya biashara na Starehe katika mtaa wa Madongoporomoka kwa kuwa hawajatosheka na mali waliyonayo.
Tumbo la viongozi halishibi katika unyakuzi wa ardhi za watu. Jitu na wakubwa wenzake wanataka kunyakuwa ardhi ya wanamadongoporomoka kwa sababu hawajatosheka na ardhi walinayo. Wanataka ardhi zaidi ya ujenzi wa majengo kama njia ya kupanua mji wao ambao hauna nafasi ya majengo zaidi.
Badala ya kusahau, Moga anaendelea kukumbuka mengi kuhusu jinsi ya kupigania haki, ili ardhi ya Madongoporomoka isichukuliwe na wakubwa walio na fedha Nyingi. Hii ni kutokana na uvumi ambao hauna nafasi zaidi ya upanuzi isipokuwa hii ya mtaa huu wa makabwela.


|