Onyesha jinsi maudhui ya utabaka na mapenzi yanavyojitokeza katika hadithi ya “Mapenzi ya Kifaurongo”.
Answer Text: Onyesha jinsi maudhui ya utabaka na mapenzi yanavyojitokeza katika hadithi ya “Mapenzi ya Kifaurongo”.(Al.10)UtabakaKatika vyuo vikuu kuna matabaka mawili la walalahai na walalahoi.Kuna walio na chochote wanachokihitaji, mavazi laini ya vitambaa vya Hariri,kutoka Uingereza, Ujerumani n.k na kuna wale kama Dennis Machora wanaotandika shuka kitandani zilizozeeka na kuchanikachanika. Kuna walio na simu za thamani, vipakatalishi na Ipad na wengine kama msimulizi ana kiredio kinachotoa sauti ya chini. Kuna wanaotumiwa pesa na wazazi wao mfano, Penina anayepokea elfu tanokila wiki kukidhi mahitaji yake na kuna wale kama msimulizi ambaye hana pesa hata angalau za kununua chakula. Kuna wale ambao wazazi wao wazazi wanacho mfano Penina ni bintiye Bw Kitiwe katibu wa kudumu katika Wizara ya Fedha, lakini wazazi wake msimulizi kila asubuhi waamkapo, mipini ya majembe huwamabegani kazi yao kubwa ni kutafuta vibarua.MapenziMapenzi ya kisasa yameambatanishwa na mali na kufanywa kitu kimoja pasi mapeni hakuna mapenzi. Wanafunzi wanapoenda vyuoni kila mmoja hujiingiza katika mapenzi, kama jinsi hali ilivyosawiriwa katika jumba la makazi la MastulaHall (uk.16) kila mtu na mpenziwe. Kuna kiu cha mapenzi kinachomfanya Penina kwenda kwa Dennis Machora na kumwomba uchumba baada ya kujua jina lake. Kuna mapenzi ya dhati vyuoni, yaani hayadumu baada ya chuo; watu wanapopatana na uhalisia wa mambo kama vile kukosa kazi. Kuna mapenzi kutoka kwa wazazi: mfanomsimulizi ana mapenzi ya dhati na wazazi waliojitaabisha kwa ajili yake.