a) Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua (Alama 10)b) Fafanua sifa kumi za mzee Mago (Alama 10)
Answer Text: a) Anwani ya hadithi TUMBO LISILOSHIBA ni mwafaka kwa hadithi hii. Fafanua (Alama 10)Tumbo lisiloshiba ni hadithi iliyopewa anwani inayosadifu yanayotendeka hadithini kwa sababu:-Jiji licha ya kwamba lina majengo mengi bado linahitaji kupanuliwa ndio sababu ardhi ya wanamadongoporomoka inapangwa kunyakuliwa.-Jitu linalokuja mkahawani kwa mzee Mago lina tumbo lisiloshiba, linaagiza lipewe vyakula vyote vilivyokuwa vimeandaliwa wateja wengine, pia linakunywa chupa kadhaa za soda.-Jitu linaapa na kuahidi kuwa lingehitaji chakula maradufu zaidi siku iliyofuata. Jambo lililowashangaza kina mzee Mago na wenzake.-Jitu lilikuja siku iliyofuata kunyakua ardhi yamadongoporomoka. Hili linaashiria kuwa tumbo halishibi si chakula tu mbali rasilimali za raia kama ardhi.-Tumbo lisiloshiba linasimamia wenye mamlaka ambao hawatosheki. Wanamiliki mali nyingi lakini bado wanahitaji kumiliki kidogo walicho nacho wanyongeb) Fafanua sifa kumi za mzee Mago (Alama 10)i) Mwenye bidii – anajitahidi kupigania haki za wanamadongoporomoka.Ana mkahawa madongoporomoka.ii) Mtetezi/mpenda haki – Anatafuta wakili ambaye hajahongwa ili kutetea haki ya wanyonge.Hapuuzi uvumi kuhusu uwezekano wa vipande vyao vya ardhi kuchukuliwa.iii) Mwenye hekima/busara – Anafahamu vyema matokeo yawingu linalotarajiwa kupigania haki zao.iv) Amepevuka/mwerevu – Anafahamu uzito wa kesi unaotokana na ardhi.v) Mzinduzi – Aliwazindua wenzake na kuwapa nasaha kuhusu maendeleo.vi) Jasiri – Analijibu jiyu kwa kuliambia wanamadongoporomoka hawataondoka.vii) Mshawishi – Aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sharia.ix) Mpenda ushirikiano – Anashirikiana na wanyonge wenzake katika kutafuta uvumbuzi wa kunyakuliwa kwa ardhi yao.x) Mwenye matumaini – Aliamini ardhi ya wanamadongoporomoka itabaki mikononi mwao.