Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili
b) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili. [alama 8]
i) Samueli
c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii. [alama 8]
Kinaya
Tashhisi/ uhuishi
Sadfa
Taharuki

 (10m 52s)
4590 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili [alama 4]
-Haya ni mawazo ya Samueli.
-Ni baada ya baba yake kwenda shule ya upili ya Busukalale kushauriana na mwalimu mkuu kuhusu karo.
-Alikuwa karibu na bwawa lililopo kwenye kinamasi karibu na kwao
-Alitaka kujitosa majini afe
b) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili. [alama 8]
) Samueli
-Alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili ya Bukukalala – kwa muda wa miaka minne
-Ni Mcheshi
-Anasema, ‘Labda mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu.’
-Pia anasema kuwa babake na mamake wameumbwa kwa aina fulani ya udongo.
-Ni mwongo / laghai
-Alidanganya babake kuwa hakupata matokeo ya mtihani kwa sababu hakuwa amemaliza kulipa karo.
-Ni mwoga
-Anaogopa anapoingia ofisi ya mwalimu mkuu na anasitasita anapozungumza.
-Ana machoka na ndiyo maana akapewa jina Rasta shuleni
-Huvunjika moyo upesi.
-Kutofaulu mtihani anakuona kama ni kuwaletea wazazi wake aibu.
-Anaamua kijitosa majini ili afe.
-Hakuna maana ya kuendelea kuishi
-Ana majivuno
-Anaelewa kuwa yeye si mwerevu lakini anajua kupanga mikakati na anaamini ana bahati kama mtende.
c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii. [alama 8]
Kinaya
-Ni kinaya Samueli kupoteza miaka minne ya kwenda shule bila mafanikio.
-Samueli anamdanganya baba yake ili atembee kilomita sita kutafuta matokeo ya mtihani ilhali alikuwa amepewa matokeo yake.
Tashhisi/ uhuishi
-Nzi wa kijani wa samawati waliokula wakashiba
-Linampokea kwa vilio nao mnuko kwa kughasi unapokea kwa vigemo.
-Safu safi ya D na E ilimkondolea macho bila kupesapesa.
SADFA
- Ilisadifu kuwa siku na wakati ambapo Samueli alitoka
kujirusha majini ili afe, Siku hiyo ilikuwa tofauti kwani wachunga walipitia hapo wakiwapeleka mifugo malishoni
Taharuki
-Kuna wanafunzi waliotokea ofisini mwa mwalimu mkuu wakiwa na furaha na huku machozi yanawatoka.
-Nina alimwacha Samueli kutokana na vituko vyake au la!
-Maisha ya Samuel yaliendelea Aje?


|