Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame Bakari.

 (8m 48s)
6807 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Jadili maudhui ya usaliti katika hadithi ,’Mapenzi ya kifaurongo’ na ‘Mame Bakari.
i.Wanajamii wanawasaliti wazazi wa Dennis kwa kuwakejeli kwa sababu ya kuwa maskini
ii.Daktari Mbonga anawasaliti wanafunzi kwa kukata kuyajibu maswali yao.Kwa mfano,anajibu wanafunzi aliyemuuliza swali kuwa kama hakujua jinsi fasihi
inavyoelekeza jamii hakufaa kuwa darasani.
iii.Baadhi ya wanafunzi chuoni Kivukoni wanawasili wenzao kwa kuwacheka wanapomwomba Daktari Mabonga atumie lugha nyepesi msichana mmoja anamcheka mpaka anaanguka
iv.Penina anamsaliti Dennis Machora kwa kumwambia kwamba hawezi kuolewa na mwanamume asiye na kazi yenye mshahara mkubwa ilhali alipomtaka kuwa mchumbawe.
v. Serikali inamsaliti Dennis kwa kutompa ajira.Miaka mitatu ilikuwa imepita akisaka kazi tangu ahitimu masomo yake ya chuo.
vi.Penina anamsaliti Dennis kwa kutombakishia chakula akidai kwamba hakuwa amemwachia pesa za kununua chakula ilhali alijua kuwa Dennis hakuwa na ajira na alitoka familia maskini.
vii.Penina anamsaliti Dennis kwa kuenda kinyume cha ahadi
yake.Anapomtaka Dennis kuwa
mchumba wake anamshawishi moyoni mwake amekuwa na azma ya kumpenda mtu milele lakini anaivunja ahadi hii.
MAME BAKARI
i. Janadume linamsaliti Sara kwa kumvamia na kumbaka akitoka masomoni
ii.Beluwa anamsaliti Sara kwa kuifichua siri ya mimba yake kwao ilhali alitaka iwe siri
iii.Jamii inamsaliti mwanamke kwa kumwona kuwa mkosaji/shetani tukio la ubakaji linapotokea
iv.Mwalimu mkuu angemsaliti Sara iwapo angemfukuza kutoka shuleni licha ya kwamba hayakuwa mapenzi yake kubakwa
v.Sara anaona usaliti wa wanajamii kwa sababu anakisia kwamba wangemsusuika na kumtenga kama mgonjwa wa ukoma iwapo wangeujua ujauzito wake.
vi.Baba yake Sara anamsaliti mkewe (mamake Sara) kwa kutompa nafasi ya kujitetea nafsi yake mbele yake.
vii.Sara anauona usaliti wa babake iwapo angejua kuwa yeye ni mjamzito.Sara anaona kuwa baba yake angemfukuza kutoka nyumbani.
viii.Raia wanalisaliti janadume lililombaka Sara kwa kuliua kwa matofali licha ya kwamba lilikuwa limemwomba Sara msamaha.


|