Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi ya Kifaurongo
b) Shogake dada ana Ndevu
c) Mwalimu Mstaafu
d) Mtihani wa maisha

 (11m 48s)
10330 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Sekta ya elimu ina changamoto nyingi.Thibitisha kwa kurejelea hadithi zifuatazo:
a) Mapenzi ya Kifaurongo
i)Mapenzi: Kuna mahusiano ya kimapenzi miongoni mwa wanafunzi,Penina anamwendea Denis kutaka kuwa mpenzi wake.
ii) Utabaka chuoni: Denis Machora anajihurumia anapojilinganisha na wanafunzi wengine kutokana na hali yake ya umaskini.
iii) Kutamauka kwa wanafunzi kutokana na ugumu wa masomo.
iv) Umaskini –Denis Machora hana mahitaji ya kimsingi kama vile chakula.
v) Ukosefu wa ajira baada ya kukamilisha masomo – Denis.
vi) Wahadhiri kutowajibika: Dkt. Mabonga anafunza vitu ambavyo haieleweki.
vii) Uzembe – Wanafunzi katika chuo kikuu hawatilii maanani masomo yao.
b) Shogake dada ana Ndevu
i) Mapenzi za kiholela: Safia na Kimwana ni wanafunzi wa shule ya msingi ilhali wana uhusiano wa kimapenzi.
ii) Mimba za mapema – Wanafunzi kupata mimba wakiwa bado shuleni. Safia alipata mimba akiwa darasa la nane.
iii) Uavyaji mimba – Wanafunzi wanaopata mimba wakiwa shule wanakata shauri kuavya mimba – Safia.
iv) Vifo vya mapema–Wanafunzi wanaopata mimba wanapojaribu kuavya mimba na kuishia kufa – Safia.
v) Kutowajibika kwa wazaz katika malezi ya watoto wao: Wazazi hawajihusishi katika masomo ya watoto wao.Wazazi wake Safia hawakujua walichokuwa wakifanya chumbani Safia na Kimwana walikodai kudurusu masomo yao. (zozote tano)
c) Mwalimu Mstaafu
i) Kutamauka:Wanafunzi kujiona zuzu wasiposhika masomo,mfano,Jairo.
ii) Ubaguzi: Kufeli katika elimu kunachukuliwa kama ni kufeli maishani. Hata hawapewi nafasi ya kuzungumza mbele ya watu.Mwalimu Mosi anawashinikiza wasimamizi katika sherehe ya kustaafu kwake kumpa Jairo nafasi ili naye aihutubie hadhira.
iii) Umaskini: Watoto kufukuzwa shule kwa kukosa
vitabu vya kaida – Sabina bintiye Jairo.
iv) Mfumo wa elimu: Haushughulikii wasioshika masomo darasani- Jairo.
v) Mapenzi ya kiholela:Wanakijiji walishuku kuwa huenda Mwalimu Mosi alikuwa amemtorosha shule Sabina bintiye Jairo.
d) Mtihani wa maisha
i) Mapuuza ya wasimamizi wa elimu: Mwalimu Mkuu
anamtupia Samueli matokeo yake kama mtu anayemtupia mbwa mfupa.Alipuuza uwepo wake ofisini mwake.
ii) Wanafunzi kutembea mwendo mrefu kwenda shule za kutwa.
iii) Ukosefu wa nidhamu shuleni; Samueli alipokuwa shuleni aliitwa ‚‘Rasta‘ kutokana mahoka yake.Anawaita mahambe kama mwalimu wao mkuu.
iv) Kufeli mitihani: Matokeo ya Samueli ni D na E katika masomo yote.
v) Mapuuza ya wanafunzi: Samueli alidhani kuwa ni mwerevu ilhali hajui chochote.
vi) Taasubi ya kiume: Samueli alitarajiwa kufanya vyema kuliko dada zake.


|