Eleza sifa za wahusika wafuatao.i) Mwalimu Mosiii) Jairo
Answer Text: Eleza sifa za wahusika wafuatao.i) Mwalimu Mosi(a) Ni karimu-Anampa Jairo zawadi alizopewa katika sherehe ya kumuaga.-Anakubali mke wa Jairo na watoto wake waishi kwake.-Alimpeleka mtoto wa Jairo shule na kumnunulia kitabu.(b) Ana utu-Anasisitiza watu waliofika katika sherehe ya kumuaga na hawakufaulu maishani wapewe fursa ya kutoa hotuba.-Hakukasirishwa na yaliyosemwa na Jairo na alimpa zawadi zake zote.(c) Ana utu kwani alikubali kuishi na mke wa Jairo kwake.-Aliwafunza wanafunzi wake vizuri na mwishowe wakawa watu wenye vyeo katika jamii.(d) Ni msiri.-Alipompatia Jairo zawadi zake hakumwambia mkewe.-Alikuwa tayari kukosolewa.ii) Jairo-Alikuwa mwanafunzi wa mwalimu mstaafu-Alikuwa mtu ovyo-Hali yake ya umaskini ilimfanya amlaumu mwalimu kwa kumpa tumaini za uongo.-Hakufanya vizuri masomoni.-Alishiriki ulevi.-Aliamini pombe ilimpa raha ya kuishi.-Alikosa uwajibikaji ndiposa akampeleka mkewe na watoto wake kwa mwalimu.