Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili.
c) Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana?
d) Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.

 (5m 34s)
3335 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“... maendeleo yanadai mchango wa kila mtu, maskini na tajiri”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
-haya ni maneno ya Mago
-anawaeleza wananchi wa Madongoporomoka
-wako katika mkahawa Mshenzi wa Mago
-wanajadili kuhusu namna ya kuzuia haki isiangamizwe
b) Taja na ueleze sifa nne za msemaji katika dondoo hili.
-ana busara - anajua kupambana na wakubwa kunahitaji ushirikiano
-mwenye bidii - anajibidiisha kulinda haki na pia katika mkahawa wake
-mtetezi wa haki - anakataa mashamba yanyakuliwe anatafuta wakili mwaminifu
-mshawishi - anafaulu kuwahamasisha wanakijiji
wote kujiandaa ili hukabiliana na wanyakuzi
c) Mambo yepi mengine ambayo msemaji huhojiana na wenzake wanapokutana?
-hali ya wanamadongoporomoka - wataenda wapi wakifurushwa
-umoja / ushirikiano baina ya makabwela
-maendeleo ya madongoporomoka
-mchango wa maskini katika kuendeleza nchi mbele
d) Taja na ueleze maudhui matatu yanayojitokeza katika dondoo hili.
-umoja-wana Madongoporomoka wanao unoja wa kutetea haki zao.
-haki-haki ya wachochole inaangamizwa.
-ushirikiano-maskini kushirikiana dhidi ya maovu ya viongozi.

|