“ Naapa na mola wangu sitofanya tena biashara hii.”a). Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)b.) Tathmini umuhimu wa mzungumzaji (alama 6)c.) “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa jamii.” Huku ukirejelea hadithi hii,thibitisha ukweliwa kauli hii kwa hoja kumi (alama 10)
Answer Text: “ Naapa na mola wangu sitofanya tena biashara hii.”a. Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)i.Haya ni maneno ya Mkumbukwaii.Anamwambia Mkubwaiii.Wamo nyumbani mwa Mkumbubwaiv.Ni baada ya kubadili nia na kutotaka kutumiwa na Mkubwa kusambaza unga/dawa zakulevya kwa matejab. Tathmini umuhimu wa mzungumzaji (alama 6)Mzungumzaji ni Mkumbukwa.Ana umuhimu ufuatao;i.Ni kielelezo cha ufisadi.Anawahonga raia ili wamchague Mkubwa katika uchaguzi mkuuii.Anaonyesha maana ya methali ‘muui huwa mwema’.Amekuwa akitumiwa na Mkubwa kuuza unga lakini amebadilika na kumsutaMkubwa kwa kuendesha biashara hiyoiii.Ametumiwa kufichua masaibu ya mahabusu gerezani .Anaeleza jinsi wanavyolala sakafuni na chakula chao kuliwa na askariiv.Ni kiwakilishi cha madhara ya kuuza unga.Anatiwa mbaroni na kufungwa kwa siku tatu baada ya kupatikana na furushi na bangi.v.Ni mfano wa raia wanaondeleza uongozi mbaya .Anawahonga raia kumchaguaMkubwa aliye na kisomo duni na asiyestahili na kumwacha profesa.vi.Ametumiwa kuufichua unafiki wa Mkubwa . Anamsuta Mkubwa kwa kufungua nyumba za kurekebisha tabia za vijana mateja ilhali ndiye anayewauzia unga.c. “Biashara inayorejelewa ilikuwa na athari basi kwa jamii.” Huku ukirejelea hadithi hii,thibitisha ukweliwa kauli hii kwa hoja kumi (alama 10)i.Kufungwa – Mkumbukwa anatiwa mbaroni na kufungwa kwa siku tatu baada ya kupatikana na begi la ungaii.Kusinzia – Mkumbubwa anadai kwamba vijana wanaotumia unga wanasinzia saa zote;hivyo kuishia kutofanya kazi.iii.Vifo – Mkumbukwa anadai kwamba vijana wengiwamekufa kutokana na matumizi ya unga.iv.Ufisadi – Biashara ya unga iliendeleza ufisadi katika jamii,Mkubwa anamhonga mkuu wa polisi Ng’weng’we wa Njagu ili amfungulie Mkumbukwa aliyetiwa mbaroni.v.Wizi – Vijana mateja wanawaibia watu mitaanivi.Fujo – Vijana mateja wanazua fujo wakitumia visu na bisibisivii.Kudhoofika kwa afya – Afya ya vijana mateja imedhoofika kutokana na matumizi ya unga.viii.Kujitoga mwili – vijana mateja wanajitoga mwili.Mwili umejaa matundu kama jahazi la mtefu.ix.Kupujuka kwa maadili – Vijana mateja wanawatusi wengine.kwa mfano ,wanamwita mkubwa makande/mavi ya batax.Uzembe - Vijana mateja wamekuwa wazembe;hawafanyi kazi .Wanalaliana vichochoroni baada ya kutumia ungaxi.Vitisho – Unga umewasababisha vijana mateja kuwa wenye vitisho .Kwa mfano,wanamtisha Mkubwa kwamba wangemtoa chango.