“..Wanafunzi wa chuo kikuu si kama watoto vikembe wa shule ya chekechea…..”a) Weka dondoo hili katika muktadha wake.b) Taja na ufafanue tamathali ya usemi uliyotumiwa katika dondoo hilic) Hadithi hii inadhihirisha utegemezi wa binadamu. Fafanua
Answer Text: “..Wanafunzi wa chuo kikuu si kama watoto vikembe wa shule ya chekechea…..”a) Weka dondoo hili katika muktadha wake. (alama 4)Msemaji ni Dkt MabongaMsemewa - Wanafunzi wa somo la fasihiMahali – Ukumbi wa mhadharaSababu – Dkt Mabonga anasuta wanafunzi kwa kuwa vitegemezi baada yamwanafunzi kutaka kueleza namna fasihi inaelekeza.b) Taja na ufafanue tamathali ya usemi uliyotumiwa katika dondoo hili (alama 2)Tashbihi- Si kama watoto wakembec) Hadithi hii inadhihirisha utegemezi wa binadamu. Fafanua (alama14)Dennis Machora na wanafunzi wenzake wanangojea Dkt Mabonga amjibu mwanafunzi ili nao wapate kujuaDkt Mabonga alisema kuwa binadamu wanapiga ubwete na kugeuka kupe.Dkt Mabonga alisema kuwa binadamu hatafuti chakula.Wanafunzi wengine wanaonelea waache masomo waende kusimamia biashara za wazazi wao.Msichana mmoja alisema kwambamchumba wake ni katibu katika wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia, kwa hivyo karibuni watafunga ndoa aondokewe na adha ya masomo.Penina alikuwa anatumiwa shilingi elfu tano kila wiki na wazazi kwa matumishi. Aidha Dennis Machora alikuwa anategemea makupo wa shule kujihikimu. Pesa hizo zinapoisha anahangaika.Dennis Machora aliona kuwa Penina angekujakulalamika kuwa Dennis Machora amekuwa kupe.Penina alisema kuwa hangeweza kuolewa na mwanamume asiye na kazi yenye mshahara mkubwa.