Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na ya Mapenzi ya Kifaurongo, fafanua maudhui ya utabaka. (al. 20)

 (8m 46s)
4927 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Kwa kurejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba na ya Mapenzi ya Kifaurongo, fafanua maudhui ya utabaka. (al. 20)
Utabaka – Tumbo Lisiloshiba
-Kuna tabaka la mabwenyenye(jitu) na lile la wanyonge(wakazi wa madongoporomoka).
-Tabaka la mabwenyenye linaendesha dhuluma dhidi ya
wanyonge k.m jitu kubwa linasimamia ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporomoka.
-Tabaka la mabwenyenye linatumia vyombo vya dola kama askari wa baraza la mji na askari polisi kuwakandamiza wanyonge.
-Ardhi ya wakazi/watu wa madongoporomoka inatwaliwa na mabwenyenye.
-Wana sheria wamezibwa midomo kwa fedha za mabwenyenye.
-Tumbo lisiloshiba linaashiria wenye mamlaka ambao hawatosheki na wanataka kunyakua kile kidogo walichonacho wanyonge.
Mapenzi ya Kifaurongo
-Wazazi wa Dennis Walikuwa wachochote na hawakuwa na mali yoyote.
-Dennis alikuwa mwanachuo wa tabaka la chini. Umaskini uliostakimu kwao hauna mfano.
-Kila asubuhi waamkapo, mipini ya majembe huwa mabegani mwa wazazi wa Dennis kutafuta kibarua cha kuwalimia matajiri mashamba.
-Dennis anayamezea mate magari makubwa makubwa ya watu wenye nacho.
-Dennis alihizika akiwa chuoni kutokana na umaskini wake
anapowatazama wanafunzi wenzake walivyonenepa na kuwanda. Mavazi yao ni laini kutoka Uingereza, Ujerumani,Marekani, na Ufaransa.
-Wanafunzi wa tabaka la juu wana simu za thamani, wengine wanabeba vipakatatahishi na ipad.
-Wanafunzi hao walisomea shule za upili za hadhi kubwa – za mikoa au za kitaifa.
-Penina kumsikitikia Dennis kutokana na hali yake duni ya ufukara.
-Tofauti ya matabaka iliwatia kiwewe wazazi wa Dennis na wale wa penina.
-Penina kusema kuwa hawezi kuolewa na mwanamume asiye na kazi yenye mshahara mkubwa.
-Shakila alikuwa na tabaka la juu. Mama yake alikuwa mkurugenzi mkuu wa shirika la uchapishaji.


|