“Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula”(a) Eleza mukadha wa dondoo hili.(b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika.(c) Eleza umuhimu wa mnenaji.(d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza” Kwa kudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli hii.
Answer Text: “Hatuwezi kumaliza kula, kila leo tunakula”(a) Eleza mukadha wa dondoo hili.(i) Mnenaji ni Mbura.(ii) Mnenewa ni Sasa.(iii) Wakiwa nyumbani kwa Mzee Mambo.(iv) Walikuwa wamehudhuria sherehe kwa Mzee Mambo bila ualishi katika siku ya kusherehekea siku ya kuingia darasa la chekechea kwa mtotowa Mzee Mambo na mwingine kutoa vijino viwili. Wanafika shereheni kula, hata hivyo wanakula kilafi mpaka Mbura anaanza kujilaumu pamoja na mwenzake Sasa, kwamba wanakula vyovyote wavipatavyo bila kuvichunguza na hata kuvila vya wenzao waliowatangulia na watakaozaliwa.(b) Fafanua tamathali ya usemi iliyotumika.Istiari / Jazanda - Wanakula lakini hawawezi kumaliza kula - wanakula kila leo na bado wanaendelea kula.(c) Eleza umuhimu wa mnenaji.Umuhimu wa mbura.(i) Ni mfano mzuri wa watu walafi katika jamii.(ii) Ni kielelezo cha watu wanaofanya kazi ngumu na nzito lakini kufaidi mapato duni.(iii) Ni mfano wa watu walio na mapuuza. Wanafahamu uzembe uliopo miongoni mwa wafanyikazi wa serikali na unyakuzi wa mali ya umma, lakini hawachukui hatua mwafaka.(iv) Ni kielelezo cha wanyonge katika jamii: Wanafaidi mabaki baada ya matajiri kujitwalia vyao.(d) “Lakini nakwambia tena, kula kunatumaliza” Kwakudokeza hoja kumi, jadili ukweli wa kauli hii.(i) Vingozi wa mataifa yanayoendelea kutowajibikia kazi zao. Wanakubali bidhaa duni kurudidikwa katika mataifa yao: mchele wa basmati.(ii) Mali ya umma kunyakuliwa: DJ anafungua duka la dawa zilizotolewa katika bohari ya serikali huku wanyonge wakiteseka.(iii) Serikali kuwalipa watu ambao hawafanyi kazi mishahara kubwa hivyo kudhoofisha uchumi wa nchi - Mzee Mambo.(iv) Kituo cha televisheni ya taifa kutumika kupeperusha matangazo ya sherehe ambazo hazina umuhimu wowote katika ujenzi wa taifa.(v) Wananchi wengine badala ya kuchukua hatua mwafaka dhidi ya wanyakuzi, hungojea wakati wao ili nao wanyakue: Sasa na Mbura “... na sisi tuende - tusogee.(vi) Viongozi wananyakua mali ya mabilioni kwa hila na hawajali: Mzee Mambo anaandaa sherehe kubwa kwa sababu mtoto wake wa kwanza ameingia shule ya chekechea na yule wa mwisho ameota vijino viwili.(vii) Watu walio karibu na viongozi kupewa vyeo ilhali wanyonge hawana kazi: Mzee Mambo ana vyeo viwili.