Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Huku ukirejelea hadithi za:
i) Mapenzi ya kifaurongo
ii) Shogake dada ana ndevu
iii) Mame Bakari
Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa. (Alama 20)

 (8m 44s)
8800 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Huku ukirejelea hadithi za:
i) Mapenzi ya kifaurongo
ii) Shogake dada ana ndevu
iii) Mame Bakari
Fafanua maudhui ya mapenzi kama yanavyosawiriwa. (Alama 20)
a) Mapenzi ya kifaurongo
i) Mapenzi dhati
- Dennis anampenda Penina kwa dhati.
- Anamtambulisha kwa wazazi wake.
- Anatazamia kumuoa haswa pindi atakapopata kazi.
- Wazazi wa Dennis wana mapenzi kwa mwanao k.m wanajitahidi kufanya vibarua vya kuwalimia matajiri mashamba ili wakimu mahitaji yake.
ii) Mapenzi kifaurongo
- Mapenzi ya Penina kwa Dennis si ya dhati. Licha ya wao kuishi pamoja anasema
kuwa hawezi akaolewa na mtu asiye na mali.
- Dennis anapokosa kazi Penina anamfurusha.
- Anamdharau na kumnyima chakula kwa sababu hakuchangia chochote kununua chakula.
- Wanafunzi wa chuo cha kivukoni wanaonekana wengi wao kuwa na mahusiano ya kimapenzi k.m huonekana wakiongozana mvulana na
msichana kufanya starehe za hapa na pale.
b) Shogake dada ana ndevu
mapenzi ya dhati
-Pana mapenzi ya dhati kati ya bwana Masudi na Bi Hamida – wanazungumza mambo mazito na ya ndani kila jioni wakisubiri usingizi uwachukue.
- Bwana Masudi na Bi. Hamida wanampenda binti yao. Upendo huu unadhihirika
kwa nama ambavyo wanamlea kwa makini.
- Wanahakikisha binti amekuzwa kwa maadili mema.
- Bwana Masudi na Bi. Hamida wanadhamini masomo kwani wanampa binti yao msaada unaohusiana na masomo kadri ya uwezo wao.
Mapenzi ya uongo
- Mapenzi kati ya Sofia na Kimwana ni ya uongo – Sofia anaposhika mimba wanajaribu kuavya jambo ambalo linasababisha kifo chake.
c) Mame Bakari
mapenzi ya dhati.
- Wazazi wa Sara walimpenda kwa dhati – kwani hata baada ya wao kujua kuwa ni mja mzito hawakumfokea.
- Anapojifungua wazazi wake wanampokea vyema. Pana mapenzi ya dhati kati ya Sara, Beluwa na Sarina. Baada ya Sara kuwaeleza yaliyomfika walimsaidia.


|