“Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.”a) Eleza muktadha wa dondoo hilib) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili. [alama 8]i) Samuelic) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii. [alama 8]KinayaTashhisi/ uhuishiSadfaTaharuki
Answer Text: “Acha nijiondelee duniani niwaachie wafanisi wafanikiwe.”a) Eleza muktadha wa dondoo hili [alama 4]-Haya ni mawazo ya Samueli.-Ni baada ya baba yake kwenda shule ya upili ya Busukalale kushauriana na mwalimu mkuu kuhusu karo.-Alikuwa karibu na bwawa lililopo kwenye kinamasi karibu na kwao-Alitaka kujitosa majini afeb) Fafanua sifa za mhusika katika dondoo hili. [alama 8]) Samueli-Alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili ya Bukukalala – kwa muda wa miaka minne-Ni Mcheshi-Anasema, ‘Labda mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu.’-Pia anasema kuwa babake na mamake wameumbwa kwa aina fulani ya udongo.-Ni mwongo / laghai-Alidanganya babake kuwa hakupata matokeo ya mtihani kwa sababu hakuwa amemaliza kulipa karo.-Ni mwoga-Anaogopa anapoingia ofisi ya mwalimu mkuu na anasitasita anapozungumza.-Ana machoka na ndiyo maana akapewa jina Rasta shuleni-Huvunjika moyo upesi.-Kutofaulu mtihani anakuona kama ni kuwaletea wazazi wake aibu.-Anaamua kijitosa majini ili afe.-Hakuna maana ya kuendelea kuishi-Ana majivuno-Anaelewa kuwa yeye si mwerevu lakini anajua kupanga mikakati na anaamini ana bahati kama mtende.c) Fafanua mbinu zozote nne za kifani katika hadithi hii. [alama 8]Kinaya-Ni kinaya Samueli kupoteza miaka minne ya kwenda shule bila mafanikio.-Samueli anamdanganya baba yake ili atembee kilomita sita kutafuta matokeo ya mtihani ilhali alikuwa amepewa matokeo yake.Tashhisi/ uhuishi-Nzi wa kijani wa samawati waliokula wakashiba-Linampokea kwa vilio nao mnuko kwa kughasi unapokea kwa vigemo.-Safu safi ya D na E ilimkondolea macho bila kupesapesa.SADFA- Ilisadifu kuwa siku na wakati ambapo Samueli alitokakujirusha majini ili afe, Siku hiyo ilikuwa tofauti kwani wachunga walipitia hapo wakiwapeleka mifugo malishoniTaharuki-Kuna wanafunzi waliotokea ofisini mwa mwalimu mkuu wakiwa na furaha na huku machozi yanawatoka.-Nina alimwacha Samueli kutokana na vituko vyake au la!-Maisha ya Samuel yaliendelea Aje?