Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya.
(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.

 (7m 30s)
2829 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“Kesho kama sote tutaamka salama……….kama tutafungua milango ya nyumba zetu”….
(a) Eleza muktadha wa dondoo hili
-Maneno yalisemwa na jitu
-Anamwambia mzee Mago.
-Wako kwenye hoteli ya mzee Mago.
-Alikuwa amemaliza kula na alikuwa akidokeza kuwa keshoye angefika pale
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumiwa katika dondoo hili.
-Takriri – Kama … kama
-Mdokezo . salama …..
-Ubashiri
-Kama tutafungua milango ya nyumba zetu.
(c) Eleza sifa sita za msemaji wa maneno haya.
-Mlafi – anakula chakula chote kwenye mkahawa.
-Mwenye tamaa – anatamani ardhi ya madongoporomoka.
-Mdunishaji – Maslahi ya wengine hawajali wanamadongoporomoka watahamia wapi.
-Mwenye upeo mfupi – Hakufikiria kuwa wanamadongoporomoka wangeweza kupingana naye na kukatia hapo.
-Mwenye dharau – Anamtamkia mzee Mago kwa
ujeuri na kusema ‘Nimekuahidi kuja kula ardhi yako hii leo’.
(d) Hadithi hii inaakisi mambo mengi yanayotendeka katika bara la Afrika.
Taja mambo sita
i) Ufisadi – Matajiri wamenyakua mali ya umma.
(ii) Unyakuzi wa ardhi – mwenye tumbo lisiloshiba anataka kunyakua mashamba ya anamadongoporomoka.
(iii) Nyakanyaka za nyumba – Nyumba nyingi sana zimejengwa kila mahali jijini.
(iv) Matumizi mabaya ya vyombo vya dola – askari wanatumiwa kawalinda mabwanyenye wanaonyakua ardhi.
(v) Ubomoaji wa vibanda – vibanda vya kina yahe vinabomolewa huko madongoporomoka.
(vi) Utabaka - Kuna matajiri na maskini. Matajiri wanaishi jijini nao maskini wanaishi madongoporomoka.


|