Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ”Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba
Kauli hii inarejelea unyanyasaji wa Wanamadongoporomoka.
Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.

 (8m 17s)
3320 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“ Hakikubakia hata chakula kidogo cha sadaka ya mwenye njaa… ”
Thibitisha ukweli wa kauli hii kwa hoja kumi ukirejelea hadithi ya Tumbo Lisiloshiba
Kauli hii inarejelea unyanyasaji wa Wanamadongoporomoka.
a) Jitu linamaliza chakula chote kwenye Mkahawa Mshenzi bila kuwajali wateja waliokuwa pale.
b) Vibanda vya Wanamadongoporomoka vinabomolewa bila kujali watapokwenda wenye vibanda.
c) Wakubwa wanaweka vikwazo katika sheria kwa makusudi ili kuwazuia watu wadogo kutetea mali zao.
d) Wanamadongoporomoka hawahusishwi katika mipango ya maendeleo katika eneo lao.
e) Askari wa baraza la mji na jeshi la polisi wanatumiwa kuwafurusha Wanamadongoporomoka
wenye njaa katika makazi yao badala ya kuwahakikishia usalama wao.
f) Majengo mengi yanajengwa katikati ya jiji kiwango cha mtu kukosa nafasi ya kuvuta pumzi.
g) Wanasheria kukosa kuwa waaminifu wanapokabiliwa na sheria ngumu.’’siku wanasheria waaminifu ni adimu kama haki yenyewe!’’
h) Wakubwa wanataka kunyakua ardhi ya wasiokuwa na nguvu kwa lazima baada ya
i) Wakubwa wanataka kuwahonga kwa visenti vyao vichache ili waondoke ilhali hawana pa kwenda.
Jadili uhalisia wa hadithi ya Tumbo Lisiloshiba katika jamii ya leo kwa kutoa hoja kumi.
a) Ubinafsi- Kuna ubinafsi na ulafi katika jamii ya kisasa kama ilivyo katika hadithi.Jitu linamaliza chakula chote kwenye Mkahawa Mshenzi bila kuwajali wateja wengine.
b) Unyakuzi- Wakubwa wanataka kunyakua ardhi ya watu wadogo kama ilivyo katika jamii ya leo ambapo viongozi hunyakua ardhi ya watu maskini.
c) Dhuluma- Wananchi hukandamizwa kwa kubomolewa vibanda/makazi yao hata bila ilani na kuachwa wakihangaika jinsi ambavyo inafanyikia Wanamadongoporomoka.
d) Ufisadi- Wakubwa wanataka kuwahonga na vijisenti vidogo ili wahame makazi yao jinsi viongozi katika jamii ya leo huwahonga wananchi maskini na kunyakua mali yao.
e) Sheria zenye vikwazo- Katika jamii ya leo,sheria huwapendelea matajiri na viongozi kwani wao huweka vikwazo makusudi ili kuwazuia maskini na wasio na nguvu kutetea haki zao.


|