Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

Alifa Chokocho : Tulipokutana tena “ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii.
iii)Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”

 (11m 12s)
11459 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Alifa Chokocho : Tulipokutana tena
“ Mamangu siku ile aliniamsha mapema.”
i) Eleza muktadha wa dondoo hili.
i. Haya ni maneno ya Bogoa Bakari.
ii. Anawaambia mkewe Sakina, Sebu na mkewe Tunu, Kazu na mkewe Bi Tunu
iii. Wamo katika kilabu ya pogopogo.
iv. Bogoa anawasimulia hadithi kuhusu jinsi alivyotolewa
nyumbani kwao na kupelekwa kwa Bi. Sinai aliyemtesa sana
ii) Tathmini umuhimu wa usimulizi wa mzungumzaji katika kuendeleza dhamira ya hadithi hii.
i. Kuchimuza suala la umaskini - Wazazi wake Bogoa hawana uwezo wa kununua sabuni / Bogoa na baba yake kutembea kwa miguu bila ya viatu hadi mjini.
ii. Kuonyesha masaibu ya wanakijiji - walikuwa na tatizo
la maji kwa maana yalikuwa hayapatikani karibu. Walitembea masafari marefu kuyatafuta.
iii. Kumfumbulia Sebu fumbo alilotaka kufumbua - Amejua sababu ya Bogoa kutoroka nyumbani kwa Bi. Sinai.
iv. Kufichua aliyempeleka Bogoa kwa Bi. Sinai - baba yake.
v. Kusawiri maudhui ya mapenzi - mapenzi ya Bogoa kwa nduguze kwa wazazi wake
yalimfanya kutotaka kutengana na familia yake.
vi. Kusisitiza kwamba Bogoa hakutaka kuishi na marafiki wa baba yake ingawa alisema kwamba ni watu wazuri– alilia na kupigwa ukwenzi.
vii. Kusawiri maudhui ya elimu - Baba yake Bogo anamwambia kwamba angepelekwa shuleni kusoma.
viii. Kuonyesha ukali wa baba yake Bogoa - Bogoa alipokataa
kuenda kwa marafiki zake mjini alimtishia kumchapa.
Onyesha jinsi mashaka linavyomwafiki mhusika mwenyewe katika hadithi ya “Ndoto ya Mashaka”
. Mashaka ni mambo magumu yanayomfika mtu katika maisha. Jina hili linamwafiki kwani ;
i. Wazazi wake wote walikufa mara tu baada ya kuzaliwa hivyo kuyakosa malezi yao.
ii. Mlezi wake Biti Kidebe anaugua miguu; hivyo inambidi amuugize ilhali yu mdogo kiumri.
iii. Anaanza kufanya vijikazi vya kuchuma karafuu na kuangua nazi akiwa mdogo kiumri ili kutafuta kipato cha kujilisha na mlezi wake Biti Kidebe.
iv. Alisoma akamaliza chumba cha nane kwa taabu na mashaka.
v. Mlezi wake, Biti Kidebe alikufa mara tu baada ya kumaliza masomo yake.
vi. Anafungishwa ndoa kwa lazima. Babake Waridi, mzee Rubeya anafika walimokuwa akiwa na watu wanne na kumfungisha ndoa bila ya yeye kuwa na habari.
vii. Familia nzima ya mzee Rubeya (babake Waridi) ilikosa raha kwa sababu ya mwanao Waridi kuolewa na yeye ambaye ni maskini .
Waliaibikia ndoa hii hadi wakahamia Yemeni.
viii. Anaishi maisha ya kimaskini kule Tandale. Inambidi kufanya kazi ya ulinzi usiku ili kuilisha aila yake. Anaishi kwenye nyumba yenye paa linalovuja.


|