“…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”a. Eleza muktadha wa dondoo hili.b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.c. Onyesha mawazo yanayomwadhibu anayerejelewa na dondoo hili.
Answer Text: “…..ilmuradi mawazo yanamwadhibu sasa”a. Eleza muktadha wa dondoo hili.Ni kauli ya msimulizi wa hadithi.Inamrejelea Samueli, mwanafunzi aliyehitimu kidato cha nne.Samueli yuko katika faragha ya msalani pale shuleni alikoingia pasi na kusukumwa na haja.Hii ni baada ya kurushiwa matokeo na mwalimu mkuu na kuona kuwa amefeli mtihani.b. Fafanua sifa za anayerejelewa katika dondoo hili.. Samueli ni;i. Mwoga - Anaonesha uoga anapoingia katika ofisi ya mwalimu mkuu na anapoingia nae anasitasita ishara ya kuwa mwoga. Analemewa kuwakabili wazazi wake nakuwaeleza kuwa amefeli mtihani.ii. Mwenye majigambo : Anajigamba kuwa ana hakika atapita mtihani na kumshtua mwalimu mkuu ambaye alionesha kutokuwa na imani naye.iii. Muongo : Ana hadaa baba yake kuwa hakupata matokeo kwa kuwa hakuwa amekamilisha kulipa karo.iv. Mwenye bidii : Anasema alikuwa akitembea mwendo wakilomita 6 kuenda shuleni kila siku na kuwa alihudhuria madarasa yake vizuri.v. Bwege : Kutokana na majibu ya yale ambayo anasema anayajua, anaonyesha kuwa zuzu na si ajabu alifeli mtihani.vi. Mcheshi : Anachekesha kwa kauli yake kuhusu mwalimu mkuu na wazazi wake. Anasema kuhusu mwalimu mkuu, “ Labda mwalimu mkuu kazidiwa na maumivu. Labda anataka kufanyiwa operesheni yaubongo ama anahitaji maombi hasa atakuwa na akili razini tena” kuhusu wazazi wake anasema,“….Mama na baba wameumbwa kwa aina tofauti za udongo”vii. Mwepesi wa kukata tamaa : Kufeli mtihani shuleni anaona kana kwamba amefeli maishani.c. Onyesha mawazo yanayomwadhibuanayerejelewa na dondoo hili.i. Anasumbuliwa na kufeli mtihani. Anaona juhudi zake nyingi za kutembea kilomita sita kuenda shuleni na kuwa na mahudhurio mazuri darasani zimeshindwa kuzaa matunda.ii. Analemewa na vipi alivyofeli mtihani ilhali kuna mambo aliyoyajua na alihudhuria madarasa vizuri.iii. Anaona muda wa miaka minne, karo iliyolipwa na baba zimepotea.iv. Anashindwa kama kuanguka mtihani ina maana kuwa hajui lolote.v. Anaona kuwa baba yake hataelewa akimwambia kuwa amefeli mtihani.vi. Anaona kama amesaliti wazazi wake, ilhali yeye kama mwana wa kiume wa pekee ndiye tegemeo lao la kuwakwamua katika lindi la uchochole.