Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“Hapana cha ala, bwana. Lisemwalo lipo,kama halipo linakuja. Kumbuka msemo mabrafu wa siri ya kata iulize mtungu . Mtungi wenyewe ni mimi ……”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
b) Bainisha tamathali mbili za lugha zilitotumiwa katika dondoo hili
c) Fafanua sifa moja ya msemaji inayodokezwa na dondoo hili
d) Msemaji wa mambo haya baadaye anageuka kata na kupiga mbizi mtungini. Eleza ukitoa mfano kutoka hadithi.
e) Eleza maudhui ya malezi kama yanavyojitokeza katika hadithi ya shogaka Dada ana Ndevu.

 (8m 40s)
4459 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“Hapana cha ala, bwana. Lisemwalo lipo,kama halipo linakuja. Kumbuka msemo mabrafu wa siri ya kata iulize mtungu . Mtungi wenyewe ni mimi ……”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili.
i) maneno ya Bi. Hamida
ii) akimwambia Bwana Masudi
iii) kitandani wakingojea usingizi uwachukue.
iv) wanazungumza kuhusu Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei ambaye wanasema awe na tabia mbaya
b) Bainisha tamathali mbili za lugha zilitotumiwa katika dondoo hili
i) methali- lisemwalo lipo kama halipo linakunja. Siri ya mtungi iulize kata.
ii) tashbihi – kata iulizwe
iii)jazanda / istiari – kata, mtungi
c) Fafanua sifa moja ya msemaji inayodokezwa na dondoo hili Mbeya/ mdaku/kilimdimi kumsengenya mkadi kuwa ana tabia mbaya.
d) Msemaji wa mambo haya baadaye anageuka kata na kupiga mbizi mtungini. Eleza ukitoa mfano kutoka hadithi.
i) Hamida alianza kumchunguza mwanawe Sofia.
ii) Alianza kumshuku mwanawe kuwa ana mimba alimwona akitapika.
iii) Alimuuliza mwanawe ikiwa anaumwa na ikiwa ameenda hospitalini.
iv) Aliyashuku mabadiliko ya mwili wa mwanawe ijapokuwa hakuwa na ashahidi.
e) Eleza maudhui ya malezi kama yanavyojitokeza katika hadithi ya shogaka Dada ana Ndevu.
i) Malezi yana changamoto kubawa kwa wazazi. Watoto wao wanawadanganya – Safia kudanganya kuwa kimwana ni shogake anayekuja wasaidiane kudurusu kumbe ni mvulana.
ii) Wazazi wanajisifu kuwa wanawapa malezi mazuri watoto wao – wazazi wa Safia kujidai wanampa malezi mazuri Safia.
iii) Wazazi wanawaamini watoto wao kiasi cha kuwa hawachunguzi mambo wanayowafanya watoto. Wazazi wa Safia.
iv) Wazazi wanaamini kuwa wanawalea watoto wao kulingana na dini- Bw. Masudi anaamini kuwa Safia ni mwenye staha.
v) Wazazi wanawasengenya watoto wa wengine – Bi Hamida kusengenya Mkadi mtoto wa Habiba Cheche kusema kuwa tabia zake siyo nzuri.
vi) Wazazi wa kike/ kina mama licha ya kuwaamini watoto wao wa kike bado ni wadadisi wanachofunza tabia zao za watoto wa kike.
vii) Wazazi wa Safia wanamruhusu Safia kujifungia chumbani mwake na shogake ili wasome vizuri bila kusumbuliwa na Lulu. Hili linawapa nafasi nzuri ya kufanya mapenzi.
viii) Wazazi wanaachwa katika hali ya masikitiko baada ya watoto wao kufa.- wazazi wa Safia.


|