Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“ Mwandishi wa hadithi ya Tumbo lisiloshiba ametumia mbinu ya Jazanda kwa ufanisi mkubwa.”

 (6m 23s)
8995 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“ Mwandishi wa hadithi ya Tumbo lisiloshiba ametumia mbinu ya Jazanda kwa ufanisi mkubwa.”
-Tumbo kubwa linalokula bila kujaa ni Jazanda ya vitendo vya matajiri wenye tama ajabu ya kunyakua bila kukoma mali ya maskini
-Jitu la miraba minne ni jazanda ya matajiri wakubwa ambao wanatumia nafasi yao kuwakandamiza maskini.
-Jitu linaingia kimiujiza bila kujulikana. Kuingia kwa ghafla ni Jazanda ya jinsi matajiri hawa wanavyovamia na kunyakua mali ya maskini bila kutarajiwa.
-Jitu kukalia meza inayoweza kutoshea watu wane ni Jazanda ya matajiri kuvamia na kunyakua ardhi/mali ya maskini wengi.
-Kiti kulalamika na meza kuonekana ndogo ni jazanda ya dhuluma na ukatili wa
matajiri hawa kwa wananchi wenye uwezo mdogo.
-Jimwili na tumbo kubwa lililolalia meza ni jazanda ya utajiri na uwezo wao wa kifedha. Tumbo kubwa pia ni jazanda ya uroho/ulafi wa mali/hawatosheki.
-Jitu kubwa kufagia chakula chote hotelini na kuwamalizia wengine ni jazanda ya jinsi amabavyo matajiri wanaparamia mali/ardhi ya
wananchi maskini bila kuwabakishia chochote .
-Jitu kuja kula katika hoteli uchwara ya mzee Mago ni jazanda ya jinsi matajiri yangekuja kuinyakua ardhi ya maskini.
-Kitendo cha jitu kula na kuramba sahani ni jazanda ya ulafi wa matajiri tapeli ambao tamaa yao haiwezi ikamithilishwa na chochote.


|