Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na majibu ya tumbo lisiloshiba na hadithi zingine

“Rasta twambie bwana!”
a) Weka dondoo katika muktadha
b) Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili
c) Ni kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe?
d) Je, mtihani wa maisha ni anwani faafu ya hadithi hii.

 (11m 17s)
8269 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“Rasta twambie bwana!”
a) Weka dondoo katika muktadha (ala 4)
Maneno ya wanafunzi wa shule ya Busulala.
Akimwambia Rasta/ Samueli Matandiko.
Walipokuwa shuleni.
Samueli alikuwa ametoka katika afisi ya mwalimu mkuu kuchukua matokeo yake ya mtihani. Marafiki waliomjua wanamtaka awaelezee alama zake.
b) Taja mbinu zilizotumiwa na mwandishi katika dondoo hili (ala 2)
i)Utohozi
ii)nidaa
c) Ni kwa vipi mzungumziwa anamchukulia mwalimu mkuu kama hambe? (alama 4)
Mwalimu mkuu wa shule ya Busulala hakuwahi
kumwamini Samueli hata siku moja kama anaweza kufaulu mtihani .
Mwalimu mkuu hakuamini Samueli aliposema kuwa amelipa ada mpaka alipohakikisha kwa kuangalia nyaraka na kumbukumbu zake.
Anamwonyesha Samueli dharau kwa kumrushia karatasi kama mbwa; anarejelea kile alichokuwa akifanya na kumpuuza.
Mwalimu mkuu hakumpa ushauri wowote Samueli ambo unmgemsaidia kupokea matokeo yake ambayo hayakuwa mazuri hata kidogo.
Mwalimu mkuu alimjibu Samueli kwa karaha, alipomwita kuwa ni fidhuli. Anamjibiza kwa kuuliza iwapo wanafunzi wengine wanalipa mawe au majani.
d) Je, mtihani wa maisha ni anwani faafu ya hadithi hii. (alama10 )
i. Mtihani wa Maisha ni anwani ambaayo imesawiri maudhui ya hadithi hii kwa kiwango kikubwa.
ii. Samueli anafanya mtihani wake wa shule ya upili na kuenda kuyachukua matokeo. Kabla ya kufikia zamu zake Samueli anajichunguza na kujipima iwapo ameyafanya vizuri. Mawazo kuhusu
mtihani huo yanamtawala. Alianza kuwachunguza wanafunzi waliokuja kuchukua matokeo ya mtihani wanapotoka mlangoni ili kujaribu kuona iwapo wamefaulu au la.Samueli anajaribu kujiaminisha kuwa yeye atakuwa amefaulu mtihani wakati akiwa kwenye foleni ya kuchukua matokeo.
Samueli anajiaminisha kuwa yeye ni mjanja na angemshangaza mwalimu
mkuu. Anagundua kuwa amefeli mtihani huo. Safu za alama ya D na ilimkodolea macho. Herufi hizo zilimfedhesha na akalemewa. Nyumbani baba yake aliyengoja matokeo kwa hamu hakuyapata.Samueli anadanganya kwamba ana salio la karo. Anapogundua ni uwongo anapandwa na ghamiza. Samueli anaamua kujitosa bwawani ili aondokane na athari za kufeli
mtihani huu wa kitaaluma. Hata hivyo anaokolewa na mpita njia.Mama yake anamwambia kuwa ingawa amefeli mtihani wa shule, asikate tamaa, bado ana mtihani wa maisha ambao anaweza kufaulu. Anwani hii inafaa sana.


|