Mbinu za lugha katika hadithi ya Mapenzi ya Kifaurongo
Answer Text: Mbinu katika hadithi ya “Mapenzi ya Kifaurongo”Taharuki-Kuna taharuki, wakati mlango wa Dennis unapogongwa: Mja huyo ni nani, Penina alijuaje kuwa huyu kijana anaitwa Dennis.-Wakati kisa kinapomalizikia pia kuna taharuki: Je Dennis alienda wapi? Alipata mastakimu vipi bila fedha?Penina aliendelea kuishi katika nyumba ile.Balagha-mbinu ya maswali yasiyohitaji jibu moja kwa moja-Wavulana wangapi wamejikuta wakining'inia bila kupenda kwao'?-Kwani swali langu liko vipi? Kwa nini wanafunzi anacheka? Maswali hayayanamhusu Dennis. Kwa nini ninalia sasa-Fukara aliyefukarika mpaka mwisho aseme nini mbele ya wanaojigamba na kujishaua?Tashbihi-ulinganisho usio wa moja kwa moja-Ninahangaika kama kondoo aliyevamiwa na jeshi la usubi-Nimetoka ofisini kama mgonjwa mahututi.-Nimeweweseka kama ubua-Mapenzi ni matamu kama uki.Yametengana kama ardhi na mbinguMethali-Mzoea sahani vya kigae haviwezi-Ujapokosa la mama hata la mbwa huanwa-Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura-Mtu huvuna alichopandaMisemo-Hazipunguzi hazizidishiUtabiri-mbinu ya kubashiri mambo kabla ya kutokea-Dennis alitabiri vile ambavyo Penina alimpenda wakati huo" akasema kesho anaweza kuwa chanzo cha kero na usumbufu. Hubalitakuwa limekufa na kufukiwa kaburini.-Hili lilitokea baada ya kukaa kwa miaka miwili na mchumbake Penina.Litifai-huu ni unukuzi wa makala mengineKuna maneno yaliyodondolewa katika riwaya ya utengano "Na nyumba hii uione paa"Kuchanganya ndimi-Your competence is doubtful,-TarmackingMjadala wa nafsi/uzungumzi nafsia-Dennis anapofukuzwa anajizungumzia sijui kama mimi ndiye kupe au mlazadamu.