Maudhui katika hadithi fupi ya Mapenzi ya Kifaurongo
Answer Text: Maudhui katika hadithi fupi ya “Mapenzi ya Kifaurongo”(a) Matabaka-Dennis anatoka katika familia maskini. Wazazi wake walikuwa wachochole, hawakuwa na mali yoyote. Walijitahidi sana kutoka katika ufukwe huo haikuwezekana. Shakila alikuwa tabaka la juu. Mama yake alikuwa mkurugenzi katika shirika la uchapishaji.Wanachuo waliotoka tabaka la juu walikuwa na maisha mazuri, libasi (nguo) zao ni bora, wana simu nzuri, tarakilishi na vitu vingine. Dennis mavazi yake, yalikuwa duni, kula kwa shida na kadhalika.(b) Umuhimu wa kazi.-Kila binadamu lazima afanye kazi. Kazi humzatiti binadamu. Kitendo cha Dennis kukosa kazikinamfanya aonekane kama mzigo asiye na faida yoyote kwa Penina. Penina anaamua kuachana naye na kumfukuza kabisa atoke kwake(c) Maudhui ya mapenzi-Wanafunzi wa Chuo cha Kivukoni wanaonekana wengi wao kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Wale wa tabaka moja huonekana wakiongozana mvulana namsichana kufanya starehe za hapa na pale.-Aidha, Penina mtoto kutoka katika tabaka la wenye nacho, anasalitiwa na mpenzi wake ambaye naye ni wa tabaka la juu. Katika kutafuta suluhisho la mapenzi ya dhati Penina anaamua kupeleka mapenzi yake kwa Dennis ambaye anatoka katika tabaka la chini.(d) Elimu-Dennis na wenzake wanasafiri hadi chuo kikuu cha Kivukoni ili kupata elimu.(e) Usalaliti-Penina anasalitiwa na mpenzi wa tabaka la juu.-Anakuja kumsaliti Dennis baada ya kukosa ajira.