Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Tumbo Lisiloshiba: Mapenzi Ya Kifaurongo (Kenna Wasike)

Muhtasari wa hadithi ya mapenzi ya kifaurongo

 (13m 35s)
8281 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
MAPENZI YA KIFAURONGO — Kenna Wasike
Muhtasari wa hadithi:
-Kifauongo ni mmea ambao majani yake hujikunyata yanapoguswa.
Dennis ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kivukoni.
-Ndani ya nafsi yake anasononeka kwa ufukara uliomwandama yeye na familia yake.
- Umaskini unamsumbua maana hali yake na ya watoto wa matajiri ilikuwa zimeachana wazi kabisa kama mbingu na ardhi.
-Kulikuwa na tofauti katika mavazi, chakula, simu na vifaa vingine vya kisasa kati yake na wanafunzi wa makabwela pale chuoni.
Dkt Mabonga alikuwa akiwafundisha. Licha ya tatizo lake la umaskini, Dennis amekabiliwa na ugumu wa somo hili. Dkt
Mabonga aliwakatisha tamaa wanafunzi wake kutokana na shutma zake kwamba wao hawafikirii na kutafakari mambo kwa kina kama wanafunzi wapevu wa Chuo kikuu.
-Alipoulizwa maswali aliwakashifu kwamba hawastahili kuwa humo kwenye darasa la chuoni.
Kwa Dennis hili liliongeza uzani zaidi wa tatizo lake.
-Wanafunzi wakwasi walipoona masomo yanatatiza
walikuwa na fursa ya kurejea makwao na kuendeleza miradi ya wazazi wao.
-Kwa Dennis hili lisingewezekana. Wazazi wake walikuwa wanategemea vibarua vya kulima mashamba ya watu
wengine. Yeye ndoto yake ilikuwa kumaliza masomo na kupata kazi ili aweze kuumaliza ukata wake na wazazi wake.
-Penina msichana wa tabaka Ia juu anamtembelea Dennis na kutaka Wawe marafiki. Dennis analipinga jambo hilo kutokana na tofauti zao za kitabaka; lakini Penina anang'ang'ania kuwa tofauti zao kiuchumi haziwezi kuwa kikwazo.
-Penina alitaka mwanaume ambaye ni mwaminifu. Anasisitiza, "Nataka tupige vita fikra kwamba kijana wa kitajiri hawezi kutangamana na mwenziwe.
Mapenzi ya Penina aliyetoka katika familia ya wakwasi na Dennis fukara yalidumu kwa miaka miwili.
-Baada ya kumaliza Chuo waliishi mtaa wa watu wastani kimapato. Pamoja najitihada zoteza kutafuta kazi. Dennis hakufanikiwa. Barua zake
nyingi alizotuma hazikumletea tumaini lolote.
-Mapenzi ya kifaurongo ya Penina yanajitokeza wazi. Anamfukuza Dennis na kumwonya kwamba nyumba yake aione paa.
Dennis alifungasha nguo zake na kuondoka akiwa haamini. Kumbe mapenzi ya Penina yalikuwa ya kifaurongo.


|