Penina na sifa zake katika hadithi ya kifaurongo
Answer Text: Penina-Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Kivukoni.-Msichana kutoka kwenye familia yenye utajiri mwingi.-Baba yake Bw. Kitime ni Katibu wa kudumu katika Wizara ya Fedha.Sifa za Penina-Ana tamaa ya mapenzi: ingawa alipewa pesa zakutosha alikuwa na majonzi kwa ajili ya kukosa mpenzi.-Ni jasiri: alimpasulia Dennis ukweli kuwa amempenda na anataka wawe wapenzi badala ya kusubiri afuatwe yeye.-Ni mnyanyapaa-Anamtupa Dennis nje ya nyumba kwa umaskini uliomvika Dennis na kutokuwa na uwezo wa kuilipia kodi nyumba.• Ni mwenye msimamo: alikata kauli ya kupendana na mwanaume asiye na pesa. Alitoa uamuzi kwamba hataolewa mpaka Dennis apate kazi kubwa. Alipokosa ajira anamfukuza na kumtukana.-Mwenye hasira: anamkasirisha Dennis kwa kashfa kali kutokana na kukosa kazi.-Mdadisi: aliweza kujua jina Ia Dennis hadi chumba chake katika Mastura Hall. Alijua kuwa Dennis hana fedha na kumweleza bayana.