Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Tumbo Lisiloshiba: Mapenzi Ya Kifaurongo (Kenna Wasike)

Ufaafu wa anwani Mapenzi ya Kifaurongo

 (5m 37s)
12535 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Ufaafu wa anwani “Mapenzi ya Kifaurongo”
-Anwani ya hadithi hii ni "Mapenzi ya Kifaurongo.
-Kifaurongo ni mmea ambao unajikunja Pindi tu unapuguswa na hujikunjua baada ya muda mfupi. Katika hadithi hii mhusika Penina anampenda Dennis kwa kuwa alikuwa mwaminifu.
- Walimaliza masomo yao lakini baada ya miaka miwili, kutokana na ukosefu wa kazi mapenzi yake yalididimia na kunyauka kabisa.
-Hakutaka kuhusishwa tena na Dennis. Alimfukuza kama mbwa.
- Ahadi zake za mapenzi zikawa kama za ule mmea.
-Dennis alihitaji kazi na alikuwa na ari ya kufaulu usaili lakini; anaulizwa swali moja tu na ananywea na kushindwa kujibu na hivyo anarudi nyumbani bila tumaini lolote.
Anaonyesha Kuwa penzi la Penina na Dennis linanyauka baada ya Dennis kukosa kazi ambayo ingempatia kipato cha kumhudumia mkewe.


|