Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa Tumbo Lisiloshiba: Mapenzi Ya Kifaurongo (Kenna Wasike)

Wahusika katika hadithi Mapenzi ya Kifaurongo: Dennis na sifa zake

 (7m 11s)
9055 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Wahusika katika hadithi “Mapenzi ya Kifaurongo”
Dennis
- Kutokana na ukata wa wazazi wake, Dennis anaishi maisha ya kimaskini chuoni.
- Anakuwa mpweke chuoni. Umaskini wake ulimfanya asijiamini na aghalabu alikuwa mwenye huzuni. Anaisikitikia hali yake duni, akawa msononevu.
Sifa za Dennis
Ni mvumilivu: anavumilia hali yao ya umasikini na ukosefu wa vifaa vya kisasa alipokuwa chuoni.
-Ana bidii: anajitahidi sana katika masomo hadi akafaulu vyema. Alisomea kijijini kwenye shule za kawaida lakini akafaulu na kuingia chuo kikuu.
-Alitafuta kazi kwa bidii, alituma tawasifu yake mahali pengi.
-Ana tamaa: alitamani awe na rafiki mpenzi kama wanachuo wengine. Kuwa na gari la kifahari-"Sikomi kuyamezea mate hayo". Alitamani hali njema ya siha mavazi bora ya watu wakwasi.
-Ni mfiitu-Anatii kauli ya Penina kumtaka aondoke
chumbani pao baada ya kukosa ajira.


|