Mhusika Bakari na sifa zake katika hadithi Mame Bakari
Answer Text: Mhusika Bakari katika hadithi “Mame Bakari”-Huyu ni baba yake Sara.Sifa zake-Anaonyesha kuwa ni mtu mkali maana binti yake anashindwa na kumweleza tukio la kubakwa shuleni.-Baadae anabadilika na kuwa mpole akampatia matunzo mtoto wake.-Ni mcha Mungu: anafanya sherehe ya Maulidi baada ya mame Bakari kuzaliwa.-Ana mlahaka mwema na majirani: anawakaribisha watu wote wakiwemo majirani kusherehekea kuzaliwa kwa Mame Bakari.-Ni mfariji: anamfariji mwanawe na kumpoza wakati alipoangua kilio katika chumba cha daktari.-Mwenye mapenzi ya dhati: baada ya kugundua kuwa Sara ana himila alimheshimu na kumwita mama.-Ni msiri: ingawaje walifahamishwa hali ya Sara mapema na mkewe, waliiweka siri na hawakuonyesha kama walifahamu chochote hadi siku rasmi iliyopangwa.Umuhimu wa Bakari katika hadithi fupi “Mame Bakari”-Kutoa msaada kwa wanaodhulumiwa. Aidha, ni kielelezo cha wazazi ambao wako tayari kubadilisha msimamo mkali wa ulezi na kutoa msaada unapohitajika.-Anawakilisha umuhimu wa kushirikiana katika malezi kwa wazazi wote wawili.-Anaonyesha heshima kitandani kwa wanawake wajawazito hata akawa hajaolewa.