Muhtasari wa hadithi ya Mame Bakari-Mohammed Khelef Ghassany
Answer Text: MAME BAKARI-Mohammed Khelef GhassanyMuhtasari-Kitoto Cha Sara ambacho kilizaliwa kilifanya baba mtu aanze kumheshimu mwanae. Sara alipata mimba iliyotokana na kubakwa.Baba yake akazidi kumpa bintiye heshima kama njia ya kumpa moyo na faraja iliyotokana na kisa hicho.-Kisa kinaanza kwa kuzingatia mashaka ya Sara msichana wa Shule ambaye alibakwa na janadume fulani. Machozi yalimkurupuka yakamwagika njia mbilimbili. Alikuwa na majuto makuu ambayo yaliandamana na mishale iliyomchoma mwilini mwake. Kila alipokumbuka kisa hicho kilitoneshakidonda kwa upya ndani mwake.-Sara alibakwa Jumatano moja usiku alikuwa ametoka kwenye masomo ya ziada. Kisa hicho Cha kinyama kilinata akilini mwake, akawa anakumbuka kila kitu. Janadume lenye harufu kali ya kutuzi lilimvamia na kumbaka ghafla. Alijaribu kujipapatua lakini akazidiwa nguvu. Likambamiza ardhini na kumkandamiza. Saraalipoteza fahamu kwa nusu saa. Alipozindukana alifahamu wazi kuwa ameshapoteza uanawali wake.-Tukio hilo la kinyama, lilimsababishia Sara majonzi si haba.Alijaribu kutatua shida yake. Akawaza na kuwazua. Hakumweleza baba yake maana alihofia hangesadiki tukio hilo na badala yake angemfukuza.-Sara alihofia vile ambavyo angeaibika kutengwa na jamii, kufukuzwa.-Shule na watu kusengenywa. Alifikiria jinsi ya kujiauni kwa aidha kujiua au kutoa mimba. Mambo hayo yote mawili hakuyaafiki.wazazi wa Sara mashaka yake kutokana na mapenzi yao wakaanza kumpa msaada. Baba mtu akaanza kumwita Sara mama.-Wakagharamia matibabu yake yote. Wakampa faraja kuu wakati Sara alipopigwa na mshangao wa kuwakuta hospitalini " Hapajaharibika jambo mama'ngu " Mapenzi ya dhati kwa mtu aliyepatwa na janga kubwa kama hili ni tiba mjarabu.