Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Mame Bakari (Mohammed Khelef Ghassany)

Mbinu za lugha katika hadithi fupi “Mame Bakari”

 (14m 37s)
5050 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mbinu katika hadithi fupi “Mame Bakari”
(a) Taswira.
-Kuna taswira ya chemchemi ya majonzi ya Sara ilipomwaga mito miwili. Inaonyesha huzuni na majonzi makuu aliyokuwa nayo.
-Kitumbo chake kilichokwishaanza kufura. Hii ni inaonyesha mabadiliko ambayo yalijilazimishia kwa Sara baada ya kubakwa.
-Kuna taswira chafu ya janadume lililombamiza ardhini.
(b) Mjadala wa nafsi/ uzungumzi nafsia
-Baada ya janga la kubakwa kumfikia Sara alikuwa na mjadala mrefu wa nafsi. Sara alijizungumzia mwenyewe ili kutafuta ufumbuzi alipohakiki chanzo cha yeye kufikiwa na janga hilo. Mfano: “yeye ni mkosewa si mkosa.
Ni mdeni si mdaiwa.
Ni mdhulumiwa si dhalimu”
(c)Mbinu rejeshi / kisegere nyuma
-Sara anarejelea Jumatano moja saa tatu na nusu akitoka stadi za ziada wakati alipobakwa. Aidha, anakumbuka daima sura mbaya ya nduli aliyembaka na yale yote aliyopitia.
-Sara anakumbuka shairi la 'Usiniuwe' alilosoma shuleni na yeye akawa mtetezi sana darasani.
-Sara na Sarina wanakumbushana vile ambavyo waliapa kusaidiana wawili Pindi wapatapo shida " Ahadi ya kale ni ile ile Sara"
(d) Sadfa
-Ilikuwa sadfa kwa Sara kuwa mtetezi wa shairi la usiniuwe
na siku mbili baadaye anabakwa. Na yeye akawa katika njia panda ya kutoa mimba au la "Sitakuua mwanangu kamwe"
-Wakati Sara alipobakwa ilisadifu kuwa uzazi wake ulikuwa sawa akashika mimba. Hii ni sadfa.
(e) Balagha
-Haya ni maswali yasiyohitaji majibu. Ni kauli za kuleta
uzindushi. Udhaifu na unyonge si ndio maana ya uanauke? Si kwa sababu ya umbile langu ndio mwili wangu ukatumiwa kukidhi utashi wao.
-Kwa nini hakutoa taarifa siku ile "Ati umebakwa? Nani akubake wewe?"
(f)Tashbihi
“….Wengi mno " na kumtenga kama mgonjwa wa ukoma.
(g) Jazanda-haya ni matumizi ya fumbo katika uandishi.
Mzigo kupata wachukuzi tatizo likapata ufumbuzi.
(h) Sitiari-Ulinganisho wa moja kwa moja.
Mwanamke ndiye shetani.
(i) Taharuki-mbinu ya kuacha wasomaji na maswali akilini.
Kuna taharuki mwanzo wa kisa hiki. Msomaji haelewi nini Sara ana majonzi mpaka asome kisa zaidi "Je, lile ndul bakaji lilifumaniwa vipi na kulifululiza hadi karibu na
Sara "


|