Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Mame Bakari (Mohammed Khelef Ghassany)

Wahusika na sifa zao katika hadithi fupi Mame Bakari-Mohammed Khelef Ghassanny

 (6m 24s)
5928 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Wahusika na sifa zao katika hadithi fupi “Mame Bakari”-Mohammed Khelef Ghassanny
Sara
Msichana wa Shule ambaye alibakwa akiwa ametoka kwenye stadi za jioni. Msichana mwaminifu ambaye amejitunza vema. Kitendo hicho kinamsononesha mno, hasa
ilipoto kwamba jibakaji hilo lilimpachika mimba.
Sifa zake
-Ni mwenye kupenda masomo: -anarudi shuleni jioni kupata masomo ya ziada anapobakwa.
-Ni mwoga: aliogopa ukali wa baba yake baada ya kutendwa unyama na hakusema kwamba alibakwa kwa ukali wa babake.
-Ana mapenzi ya dhati: yeye na Sarina wanapendana sana na wanaapa kwa hali yoyote ile.
-Ana busara: anaamua kuwa kujiua sio suluhisho mwafaka maana yeye siye aliyekosa na kuomba msaada wa rafikiye Sarina.
-Ana utu: hakutaka kuavya mimba kwa hivyo akakihifadhi kitoto chake tumboni.
-Ni mwelewa wa jamii yake: alijua vile watu walivyo wanapenda kudodosa mambo ya wengine.


|