Maudhui makuu katika hadithi fupi, Mame Bakari-Mohammed Khelef Ghassany
Answer Text: Maudhui makuu katika hadithi fupi, “Mame Bakari”-Mohammed Khelef Ghassany(a) Siri- Mtu anapopatwa na shida nzito huhitaji kuiweka siri hadi wakati mwafaka. Sarina alitunza Siri ya Sara kwamba ni mja mzito. Aidha walipomweleza Beluwa naye aliahidi kuiweka Siri. Daktari Beluwa aliweka siri lakini akawa ametafuta dawa boraZaidi ya kuwaeleza wazazi wao.(b) UhalifuYule nduli ambaye ndiye baba mtoto wa Sara, alitenda tendo la kinyama kwa msichana. Msichana mnyonge na dhaifu, alijaribu kupigana nalo likamshinda nguvu. Hata hivyo uhalifu haulipi chochote. Alimdhulumu Sara na kutoroka akamwachaamezirai nusu uchi. Unyama huo unafikia mwisho wakati alipojaribu kubaka msichana mwingine.Aliadhibiwa vikali akaupoteza uhai wake.(c) KifoKuna kifo ambapo janadume lililombaka Sara linauliwa karibu na pao. Sara mwanzoni pia anapania kukiavya kitoto chake.(d) MaleziWazazi wake Sara wanamlea kwa penzi licha ya tatizo lililompata la kubakwa na kupata mimba mapema.(e) ElimuTwapashwa kwamba Sara alikuwa msomi aliyebakwa akienda masomo ya ziada.