Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na Majibu Katika Riwaya ya Chozi La Heri

Jadili maudhui ya nafasi ya mwanamke katika jamii (alama 20).

 (7m 34s)
25083 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Jadili maudhui ya nafasi ya mwanamke katika
jamii (alama 20).
Jibu.
- Mwanamke amesawiriwa kwa namna mbalimbali:
- Mwanamke ni Msomi-Tila alikuwa akimudu masuala ya sheria.
- Hakuna aliyethubutu kuuchangia mijadala kwani katika masuala ya sheria Tila alikuwa ameyamudu kweli kweli.
- Selume- Ridhaa alimfariji na kumwomba asilie kwani mwana wake yu hai tena ana kisomo na amehitimu kama mkunga, anaweza kujitegemea.
- Umulkheri pia alisoma na kuhitimu vizuri.
- Mwanamke ni Mjinga- Tuama alikuwa amejipata katika hali mbaya kwa kukubali kupashwa tohara. Alibahatika kwa kuwa hakuiaga dunia kama wenzake. Tuama anaitetea mila hii ya upashaji tohara kwa wanawake eti haijapitwa na wakati kwani bila tohara mwanamke hubakia kuwa mtoto. Huu ni ujinga na upumbavu.
- Mwanamke ni mwenye bidii- Tunaelezwa kuwa Umulkheri alikuwa nyuma yake Dick akiwa amepiga foleni. Anasafiri ng'ambo kwa shahada yake ya uhandisi katika masuala ya kilimo. Umu, baada ya kuchukuliwa na Mwangeka na Apondi alifanya bidii masomoni na kufuzu vyema katika mitihani yake.
- Mwanamke ni mwenye tamaa ya mali- Naomi hakuwekwa na mazingira haya mapya(Mlima wa Simba).
- Mwanamke ni katili/muuaji- Mamake Sauna alimsaidia Sauna kuavya mimba aliyokuwa amepachikwa na babake mlezi. Neema naye alikuwa ameavya mimba nyingi akiwa kwenye Chuo kikuu.
- Mwanamke ni mwenye majuto- Neema alikuwa mwenye kujuta kwa kupoteza nafasi ya kupanga mtoto.
- Mwanamke ni mwenye kujiheshimu- Zahali amewahi kupigana na majitu yaliyokuwa yakitaka kuuhujumu utu wake kwa kumnyanyasa kijinsia.
- Mwanamke ni mcheshi- Terry ambaye kawaida yake ni mcheshi hakunyamaza bali alimwambia Ridhaa kuwa kwake lazima kila jambo liwe na kiini.


|