Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na Majibu Katika Riwaya ya Chozi La Heri

Jadili maudhui ya 'asasi ya ndoa' kama yalivyoangaziwa riwayani (alamo 20).

 (7m 8s)
9250 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Jadili maudhui ya 'asasi ya ndoa' kama
yalivyoangaziwa riwayani (alamo 20).
Jibu.
- Ndoa ni maafikiano rasmi baina ya mwanamume na mwanamke ili waweze kuishi pamoja kama mke na mume.
- Ridhaa alikuwa na mke kwa jina Terry. Walibarikiwa kuwa na watoto wafuatao: Mwangeka, Tila na marehemu Dede. Ndoa hii haikudumu kwani janga la moto iiliisambaratisha aila hii na ndipo Terry, Tila, Lily na Becky wakaiaga dunia. Ridhaa akabaki mjane.
- Mwangeka alikutana na Lily Nyamvula katika chuo kikuu na kumwoa. Walibarikiwa na mtoto mmoja kwa jina Becky. Ndoa hii haikudumu kwani Lily na Becky waliangamia kwenye janga la moto.
- Baada ya ndoa ya mwanzo kusambaratika, Mwangeka Alimwoa Apondi. Walibarikiwa na mwana wa kiume kwa jina Ridhaa.
- Mwangemi alimwoa mwanamke kwa jina Neema. Hawakufaulu kupata mwana wao kindakindaki japo walipanga mwana wao kwa jina Mwaliko.
- Kangata alikuwa na mke wake kwa jina Ndarine.
Walibarikiwa na wana wafuatao: Lunga Kiriri, Lucia Kiriri na Akelo Kiriri. Lucia Kiriri Kangata – alikuwa ameolewa katika ukoo wa Waombwe ambao awali walikuwa maadui sugu wa ukoo wao.
- Kaizari alikuwa na mke kwa jina Subira. Walibarikiwa na mabinti wawili, Lime na Mwanaheri.
- Lunga alikuwa na mke kwa jina Naomi. Walikuwa na watoto watatu, Umu, Dick na Mwaliko. Ndoa hii haikudumu
- Pete na Fungo- Tunaelezwa kuwa Pete alipoingia darasa la saba alipashwa tohara nao wajombake wakapokea
posa na baadaye mahari kutoka kwa buda mmoja kwa jina Fungo aliyemuoa kama bibi wa nne. Ndoa hii haikudumu.


|