Fafanua namna mbinu ya sadfa ilivyotumiwa katika Riwaya (alama 20).
Answer Text: Fafanua namna mbinu ya sadfa ilivyotumiwa katikaRiwaya (alama 20).Jibu- Sadfa ni matukio mawili ambayo hayakupangwa kutukia wakati mmoja. Sadfa imejitokeza katika mazingira yafuatayo.- Kukutana kwa IJmu na Dick kwenye uwanja wa ndege.- Ni sadfa kuwa wakati Umu anampa Dick ushauri wakiwa katika safari, ndipo Dick alikuwa ameamua kuyabadilisha maisha yake.- Ni sadfa kuwa Mwangeka ndiye mlezi wa Umu na Dick, naye binamu yakeMwangemi ndiye mlezi wa Mwaliko. lkumbukwe kuwa Umu, Dick na Mwaliko ni ndugu.- Ni sadfa kuwa hoteli aliyoichagua Mwaliko kumpeleka babake ili amnunulie chakula cha mchana ndiko akina Umu walikuwa na wazazi wao.- Kukutana kwa Mwaliko na ndugu zake wawili ilikuwani sadfa. Hakujua kuwa wangekutana kwenye Hoteli ya Majaliwa.- Ni sadfa kuwa siku yake Umu ya kuzaliwa ilikuwa ndiyo siku ya kuzaliwa kwa Mwangemi.- Ni sadfa kuwa siku aliyoitwa Ridhaa kwenda kumhudumia mgonjwa ndiyo siku aila yake iliangamizwa na kumponyoka.