Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Maswali na Majibu Katika Riwaya ya Chozi La Heri

“Lakini itakuwaje historical injustice, nawe Ridhaa, hapo ulipo sicho kitovu chako?"
(a) Eleza muktadha wa dondoo.
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye dondoo hili (alama 4).
(c) Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya (alama 6)
(d) Ni mambo gani yaliyowakumba wale ambao kitovu chao sicho ( Alama 6)

 (7m 0s)
19888 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
“Lakini itakuwaje historical injustice, nawe Ridhaa, hapo ulipo sicho kitovu chako?"
(a) Eleza muktadha wa dondoo.
Jibu.
- Hayo ni maneno ya Ridhaa yaliyokuwa yakimpitia baada ya kumjibu Tila mawazoni.
Hii ni baada ya Ridhaa kukubali maneno ya Tila ya hapo awali. Inadhihirika kuwa amekubali kuwa yeye ni mgeni, si mwenyeji.
(b) Eleza tamathali mbili za lugha zilizotumika kwenye dondoo hili (alama 4).
Jibu.
Swali balagha- ...hapo ulipo sicho kitovu chako? Kuchanganya ndimihistorical injustice.
(c) Fafanua umuhimu wa msemaji wa maneno haya (alama 6)
Msemaji wa Maneno haya ni Ridhaa. umuhimu wake.
- Ridhaa ametumiwa na mwandishi kutukanya dhidi ya ukabila.
- Ridhaa ni kielelezo cha watu wasiobagua watu.
- Hakujali wanakijiji wenzake ni wa ukoo gani(uk.20). Aliifanya miradi ya maendeleo ili kuwafaidi wote.
- Ridhaa ametumiwa kuuonyesha udhalimu kwa maskini kwa namna majumba yake yalivyobomolewa.
(d) Ni mambo gani yaliyowakumba wale ambao kitovu chao sicho ( Alama 6)
Jibu
- Walichomewa nyumba zao. Kwa mfano, Ridhaa alichomewa jumba lake la kifahari.
- Watu wao waliuawa. Kwa mfano, familia ya Ridhaa ilichomwa na Bwana Kedi jirani yao. Walikimbia na kutorokea msituni.
- Watoto wao walibakwa. Kwa mfano, mabinti zake Kaizari walibakwa na vijana wenzao.
- Walitoroka kuacha makwao wakawa maskwota au wakimbizi.

|