Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za kiafrika.Tetea kauli hii ukirejelea chozi la heri (alama 20).
Answer Text: Ukabila ni tatizo sugu katika nchi nyingi za kiafrika.Tetea kauli hii ukirejelea chozi la heri (alama 20).Jibu- Ukabila ni matendo au fikira za mtu za kuthamini kabila lake mwenyewe tu na kuwabagua wamakabila mengine. Ukabila umejitokeza kama ifuatavyo katika Chozi la Heri.- Subira alitengwa na familia ya mume wake kwa kuwa wa kabila tofauti na lao. Mwanaheri anatueleza kuwa mama yake alikuwa ametoka kwenye jamii ya Mamwezi lakini babake alikuwa wajamiii tofauti. Kila mara Subira aliitwa 'muki' au ‘huyo wa kuja’.- Kwa miaka mingi aliweza kuvumilia kubaguliwa, kufitiniwa na kulaumiwa kwa asiyoyatenda. Mwishowe alihiari kujiondokea na kwenda mjini alikojinywea kinywaji kikali, akafa.- Mzee Kedi alimtendea udhalimu Ridhaa na kuiteketeza aila yake licha ya wao kuwa majirani kwa miaka hamsini. Ridhaa alifanyiwa hivi kwa kuwa alikuwa ametoka kwenye kabila tofauti na Kedi.- Ami zake Kangata walimsuta mno kwa kumwoza mwanawao kwa mtu wa jamii tofauti na yao. Walishangaa ni vipi mwana wao ataozwa kwa mtu wa ukoo ambao huvaa nguo tofauti.- Waliamini kuwa ukoo huo huzaa majoka ambao hata kiporo cha juzi hayawezi kukupa.- Ndoa ya Selume ilisambaratika baada ya vita vya kutawazwa kwa kiongozi mpya. Alibakimwenye kilio baada ya wambea kumfikishia ujumbe kuwa mume wake amekwisha kuoa msichana wa kikwao.- Tulia alimsaidia Kaizari kufunganya na kumsindikiza hadi njia panda. Alimkumbatia na kumwambia kuwa mwenyezi mungu ndiye hupanga na nguvu namamlaka pia hutoka kwake. Akamjuvya kuwa uongozi mpya umezua uhasama kati ya koo ambazo zimeishi kwa amani kwa karibu karne moja.