Maovu yametamalaki katika jamii ya Riwaya ya Chozi la Heri.Tetea kauli hii kwa kutumia hoja kumi zisizopingka (alama 20).
Answer Text: Maovu yametamalaki katika jamii ya Riwaya yaChozi la Heri.Tetea kauli hii kwa kutumia hoja kumi zisizopingka (alama 20).Jibu.- Katika jamii hii kuna biashara haramu kama ileya uuzaji wa dawa za kulevya. Dick alipotekwa nyara alilazimika kuuza dawa za kulevya kwa muda wa miaka kumi.- Kuna ukabila- Suala hili la ukabila lilijitokeza kikamilifu wakati kulizuka vita vya kisiasa vya kutawazwa kwa Mwekevu.- Kuna mauaji- Watu wengi waliowapoteza wapendwa wao kutokana na migogoro iliyozuka baada ya kutawazwa kwa kiongozi mpya.- Katika jamii hii kuna matumizi ya pombe haramu – Vijana wa vyuo vikuu wanabugia pombehii ya sumu inayowafanya wengine kuiaga dunia.- Kuna ukeketaji wa watoto wa kike- Wasichana wa shule ya msingi wanapitishwa tohara. Wasichana wengine wanayapoteza maisha yao huku wengine wakiponea chupuchupu na kuwa hospitalini. Kwa mfano,Tuama anayeitetea mila hii iliyopitwa na wakati aliponea kidogo kuiaga dunia.- Kuna wizi wa mali ya wengine- Wakati vita vya baada ya kutawazwa kuzuka, watu walionekana kupora maduka ya Kihindi, Kiarabu na hata ya Waafrika wenzao.- Katika jamii hii wanawake huavya mimba- Sauna alipachikwa mimba na babake mlezi. Mamake mzazi alimsaidia kuavya kisha akamwonya dhidi ya kumwambia yeyote kuhusu unyama wa babake.- Kuna baadhi ya wazazi wanaohusiana kimapenzi na watoto wao- Sauna alipachikwa mimba na babake mlezi. Mamake mzazi alimsaidia kuavya kasha akamwonya dhidi ya kumwambia yeyote kuhusu unyama wa babake.