Mbinu katika hadithi fupi ya Kidege-Robert Oduori
Answer Text: Mbinu katika hadithi fupi ya “Kidege”-Robert Oduori(a) Taharuki-Kuna taharuki ya kujua wapi mapenzi ya Achesa na Joy yameishia. Je, baada ya bustani kuvamiwa na midege waliendelea kuvinjari eneo hilo?-Kuna taharuki ya kujua kama Mose alifanikiwa kuonana na Shirandula na kumpatia jibulake. Kama alimpa jibu, kuna taharuki ya kujua kama jibu hilo lilikuwa sahihi.(b) Tanakali za sauti, kwa mfano: .shwii shwaa shwii shwaa shwiii.(c) Misemo na nahau, kwa mfano: binadamu nao na hamsini zao.(d) Taswira, kwa mfano:Kidege-huashiria watu wanyonge katika jamiiMidege —Huashiria watu wenye nguvu za kiuchumi/kiutawala wanaowanyonga wanyonge.Visamaki — huashiria rasilimali zinazoporwa na watu,nguvu na mamlaka ya kiutawala.