Maudhui katika hadithi fupi- Kidege
Answer Text: Maudhui katika hadithi fupi “Kidege”(a) Dhuluma na UnyonyajiMwandishi anatumia midege mikubwa kubaini suala ladhuluma na unyonyaji.Midege mikubwa inavamia bustani na kuanza kula visamaki vilivyokuwa katika kidimbwi.Katika kuvizia na kunyakua visamaki, midege hii inaharibu mazingira ya bustani hiyo.Midege inajadiliana namna ya kujenga jamii. Inakubalianakuwa kujenga jamii ni kula kila kitu kinachoonekana kidogo kwao.Hii inaashiria namna wanyonge wanavyopokonywa rasilimali na tabaka lenye mabavu katika jamii.(b) MatabakaHadithi hii inabainisha kuwapo kwa matabaka mawili katika jamii ambayo yako katika mapambano.Kuna tabaka la midege mikubwa. Hii ina nguvu midomo yao ni kama mapanga.Midege mikubwa inavamia na kutwaa visamaki vilivyokuwa katika kidimbwi cha bustani ya Ilala.Videge vidogo vinajitetea kwa kuogopa kudhulumiwa na midege mikubwa. Vinaashiria wa jamii hii.(c) Umoja na Mshikamano-Hadithi hii inabainisha kuwa nguvu ya mnyonge ni umoja na mshikamano.-Videge vidogo vinaungana kwa wingi wao na kuamua kupambana na midege mikubwa.-Videge vinashikamana kuparua macho ya midege mikubwa na kuyatia sumu.-Videge vidogo vinashinda mapambano hayo na kufanikiwa kuifukuza midege mikubwa.