Dhamira ya mwandishi katika hadithi ya Kidege
Answer Text: Dhamira ya mwandishi katika hadithi “Kidege”-Mwandishi wa hadithi hii amedhamiria kubainisha kuwa umoja na mshikamano ndiyo nguzo imara ya mnyonge.- Kama wanyonge wakishikamana, kwa umoja wao wanaweza kuondosha wavamizi wote wanaowadhulumu rasilimali na haki zao.- Wanyonge hawa wanawakilishwa na videge vidogo vinavyodonoa na kutia sumu machoni pa midege mikubwa inayodhulumu visamaki vidogo.