Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Kidege (Robert Oduori)

Muhtasari wa hadithi fupi-Kidege

 (9m 23s)
4599 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Muhtasari wa hadithi fupi “Kidege”
-Hupenda kwenda kubarizi upepo na kuburudishwa kwa mandhari yake. Joy na Achesa wanaonekana wakivinjari mahaba yao katika, bustani hii. Wanagaragazana katika viunga vya bustani hii, ilimradi tu wanajifurahisha.
-Mose naye anapendelea kutembelea bustani hiyo. Katika bustani hii, kuna kidimbwi cha maji. Ndani yake visamaki vidogo vyenye rangi anuwai za kuvutia. Aidha, kidege ambacho kimezoea kuonekana hapo.
-Mose amezoea kubeba sima mfukoni mwake. Akifika katika kidimbwi hicho huvirushia visamaki sima. Wakati mwingine Mose huenda bustanini hapo na rafiki yake Shirandula. Shirandula yeye ni mzaliwa wa shamba
Shrandula anadai kuwa visamaki hivyo ni vidogo kuliko vile vilivyoko kijijini. Visamaki hivyo havifai kuvuliwa na kuliwa.
Siku moja Shirandula alimtegea Mose kitendawili. Kitendawi hicho kilitaka kujua ni yupi bora kati ya mjenga choo na mjenga kasri. Mose aliomba siku
kadhaa ili atafakari jibu la kitendawi hicho.
-Katika kutafuta majibu ya kitendawili hicho, Mose anaona midege mikubwa yenye midomo kama panga. Midege hiyo ilikuwa imekizunguka kile kidimbwi chenye visamaki vya kuvutia. Midege ile ilikuwa ikijadiliana namna ya kujenga jamii. Ndipo ikakubaliana kuwa kujenga jamii ni kula vitu vyote ambavyo yanadhani vidogo. Midege ile ikaanza kurarua vile visamaki. Mingine ilikuwa ikinyang’anyana.
-Mose anashindwa kuifukuza ile midege. Mara kinakuja kile kidege
Videge vile vinashuka kwa kasi ya ajabu na kudonoa macho ya midege mikubwa. Vinatia sumu fulani katika macho ya ile midege. Mara midege inaanza kutapatapa na hatimaye kukimbia na kutoweka.
-Mose alikuwa anashuhudia mtifuano ule wa videge vidogo dhidi ya midege mikubwa. Anafurahia kuiona midege mkubwa inafukuzwa
na videge vidogo. Hatimaye kitendawili kinateguliwa kwa Mose kugundua kuwa mwenye choo ndiye hunya na mwenye kasri hawezi.


|