Ufaafu wa anwani “Kidege”-Robert Oduori
Answer Text: Ufaafu wa anwani “Kidege”-Robert Oduori-Anwani ya hadithi hii ni; Kidege.- Anwani hii inasawiri maudhui yaliyomo ndani ya hadithi hii.- Kidege ni ndege mdogo ambaye anaashiria wanyonge wa tabaka la chini.- Wanyonge hawa wanakandamizwa kwa kudhulumiwa na midege mikubwa ambayo inaashiria tabaka la mabwana wenye nguvu. -Hadithi hii inaeleza namna videge vilivyoungana kwa wingi wao na kuifurusha midege ambayo imevamia bustani na kuanza kuvirarua visamaki vilivyokuwa kwenye kidimbwi.