Get premium membership and access revision papers with marking schemes, video lessons and live classes.
  OR
Processing. Please wait.

 Uchambuzi wa tumbo lisiloshiba: Masharti ya Kisasa (Alifa Chokocho)

Mbinu za lugha katika hadithi fupi ya Masharti ya Kisasa

 (12m 3s)
6075 Views     SHARE

Download as pdf file

Answer Text:
Mbinu katika hadithi fupi ya “Masharti ya Kisasa”-Alifa Chokocho
(i) Taharuki
Baada ya kupelekwa hospitali, Je alipona au aliaga dunia, ukizingatia kuwa aliumia vibaya kichwani. Je, Kidawa alikichukuliaje kitendo hicho cha mumewe kupanda juu ya paipu na kuchungulia ndani?.
(b) Taswira
Wakati Dadi yuko juu ya baiskeli yake akiita wanunuzi.
Kuna taswira ya Kidawa akiwa amevalia viatu vipya na kanzu tayari kwenda kazini usiku. Zipo taswira nyingine nyingi.
Aidha kuna taswira ya kile chakula cha jioni cha ndizi na samaki ambacho Dadi hakukigusa kwa wivu.
(c) Sadfa
-Dadi alienda kuona iwapo mwalimu alikuwa kwake jioni.Alipomkosa akajihakikishia kwamba alienda kukutana na Kidawa.
-Aidha ilikuwa sadfa kuwa taa ya nje ilikuwa haiwaki na Dadi akapata mandhari mazuri ya kujificha akipanda ile paipu.
(d) Kuchanganya ndimi
Kuna maneno ya Kiingereza yaliyotumika kama "Stop your gaze!" my dress my choice celeb, socialite n k.
(e) Mdokezo-maelezo ya mambo yaliyopita.
-Kidawa alijaribu kumhakikishia mumewe uaminifu wake na kumkumbusha ahadi zao, alipogeuka na kuona chakula hakikuguswa alikatisha usemi wake.
-Dadi alipokuwa akienda shuleni kumwangalia mwalimu mkuu, alijiapiza kuwa leo ni leo na hakumaliza msemo huo.
(f) Takriri
Neno kisasa limerudiwarudiwa kusisitiza kiini cha hadithii hii "Mwanamke wa kisasa hutafuta mwanaume wa
kisasa, mwenye mapenzi ya kisasa
(g) Misemo
-Nyota ya jaha
-Pweleo la tamasha
-Kugeuka maji kuzima moto
(h) Koja
Mapenzi ni mateso, ni utumwa ni ukandamizaji, ni udunishaji, ni ushabiki ni ugonjwa usio dawa.
(i) Tashbihi
…kama anga lolote Ia dunia
(j) Tanakuzi
Matumizi ya maneno yanayopingana. Waliosoma wasiosoma wenye uwezo na wasio nao.


|